INJILI YABISHA HODI IMEKUWA!!!
Katika hali ya Kustaajabisha, Injili imebisha hodi katika kijiji cha Imekuwa kilichopo mkoani Mtwara ambapo baadhi ya watu wamesalimisha maisha yao katika mikono salama ya Yesu mara baada ya kupokea mafundisho kwa njia ya redio (Info Radio) inayo rusha matangazo yake kutoka Mtwara. Wakitoa ushuhuda wao waumini hao
walisema kuwa walisikia mafundisho ya Biblia kupitia kituo hicho cha redio na baada ya kuelewa waliamua kukata shauri na kumfuata Yesu.
Waumini hao wapya walianza jitihada za kutafuta mahali kanisa la Waadventista Wasabato lilipo, ndipo walipo fanikiwa kupata mawasiliano ya mmoja kati ya wainjilisti wa kanisa na kufanikiwa kuungana na kundi kubwa la waumini waliopo Mtwara.
Hili ni jambo la kumshukuru Mungu kwani amejiinua kwa namna ya pekee katika kijiji cha Imekuwa. Mungu abariki kundi hili dogo ili likaongezeke na hatimaye kuwa kanisa.

No comments
Post a Comment