HATIMAYE EFFORT YA MTWARA SDA YAHITIMISHWA.

Mkutano wa injili uliodumu kwa majuma matatu katika viwanja vya kanisa ka Waadventista Wasabato la Mtwara mjini umehitimishwa rasmi jana tarehe 31 January 2015 siku ya Sabato. Katika Mkutano huo mkono wa bwana umetenda kazi na waumini wapatao 9 walimpokea Yesu kwa njia ya ubatizo. Aidha waumini wengine 3 toka kanisa la Ziwani pia walibatizwa na kufanya jumla ya walio batizwa kutoka Ziwani na Mtwara mjini kufikia 12. 
Mara baada ya kufungwa kwa mkutano huo mzee wa kanisa la Mtwara mjini bwana Godfrey Nyombi alitoa wito kwa waumini kujiandaa kwa mkutano mwingine mkubwa wa injili unao tarajiwa kufanyika mwezi wa 6. 


No comments

Powered by Blogger.