SABATO YA KUFUNGUA MWAKA 2015 MTWARA ILIKUWA HIVI
Kanisa la Waadventista Wasabato Mtwara limefanya ibada ya pekee kufungua mwaka 2015. Katika ibada hiyo, mchungaji wa mtaa wa Mtwara Pr. Zetti Ndola amewaasa washiriki kujitoa katika kuifanya kazi ya Mungu mwaka huu. Mchungaji Ndola amesema hakuna haja ya kukataa kushiriki katika kazi ya Mungu pale tunapo hitajika kufanya hivyo.
Mchungaji Ndola amewakumbusha waumini kuwa Mungu anao watendakazi wengi hivyo usipo kubali kumtumikia mtu mwingine atachukua nafasi yako na hautapata mbaraka.
Mara baada ya hubiri la pekee Mchungaji Ndola alitoa wito kwa waumini kujiweka wakfu na kujirekebisha pale walipo anguka mwaka uliopita. Kwakweli Sabato ya leo ilikuwa ya pekee sana na Mungu amenena na wana na binti zake kupitia mtumishi wake Mchungaji Zeti Ndolla.
Mchungaji Zeti Ndolla akitoa wito kwa waumini |
Waumini wakiwa tayari kwa ombi la kuwekwa wakfu |
No comments
Post a Comment