Kesha la Asubuhi Ijumaa, 22/11/2019
KESHA LA ASUBUHI
Ijumaa, Novemba, 22, 2019
HERI WAZIFUAO NGUO ZAO
📖"Heri wazifuao nguo zao, wawe na amri kuuendea huo mti wa uzima, na kuingia mjini kwa milango yake"📖. Ufunuo 22:14.
✍🏻Je, tunatarajia mwishowe kufika mbinguni na kujiunga na kwaya ya mbinguni? Kuhusu tabia zetu, hali tutakayokuwa nayo tunapokufa ndiyo ile ile tunayofufuka nayo... Huu ni wakati wa kufua mavazi ya kuyanyoosha.
✍🏻Yohana aliona kiti cha enzi cha Mungu na mkutano mkubwa ukizunguka, na kisha akauliza, hawa ni nani? Jibu likatolewa, "Hao...wamefua mavazi yao, na kuyafanya meupe katika damu ya Mwana-Kondoo." ( Ufunuo 7:14 ).
Kristo atawaongoza kwenye chemchemi za maji yenye uhai, na pale pana mti wa uzima na pale yupo Mwokozi wa thamani. Hapa atawasilisha kwetu uhai ulio sawa na uhai wa Mungu. Pale hapatakuwa na maumivu, huzuni, ugonjwa, au kifo. Yote ni amani na upatanifu na upendo....
✍🏻Sasa ni wakati wa kupokea neema na nguvu na uwezo, kuziunganisha na juhudi zetu za kibinadamu ili tuweze kujenga tabia kwa ajili ya maisha ya milele. Tunapofanya hivyo tutatambua kuwa malaika wa Mungu watatutumikia, na tutakuwa warithi wa Mungu na warithi pamoja na Yesu Kristo. Na tarumbeta ya mwisho itakapolia, na wafu watakapoitwa kutoka kwenye gereza lao na kubadilishwa, kufumba na kufumbua, taji za utukufu wa kutokufa zitawekwa juu ya vichwa vya washindi. Milango ya lulu itafunguka kwa ajili ya mataifa walioushika ukweli, nao wataingia. Pambano litakuwa limekwisha.
✍🏻Njoni, mliobarikiwa na Baba yangu, urithini ufalme mliowekewa tayari tangu kuumbwa ulimwengu" ( Mathayo 25:34 ).
Je, tunahitaji baraka hii? Mimi ninahitaji, na ninaamini kuwa na wewe unaihitaji.
Hebu Mungu akusaidie ili uweze kuvipiga vita vya maisha haya na kupata ushindi siku kwa siku na mwishowe uwe miongoni mwao watakaozipata taji zao miguuni pa Yesu na kupiga vinubi vya dhahabu na kuijaza mbingu yote kwa nyimbo tamu. Ninataka wewe umpende Yesu... Usimkatae Mwokozi wangu, maana alilipa gharama isiyo na kikomo kwa ajili yako. Ninaona ndani ya Yesu uzuri usio kifani, na ninataka na wewe uone uzuri huu.
MUNGU AKUBARIKI UNAPOTAFAKARI NENO LAKE..🙏
No comments
Post a Comment