Kesha La Asubuhi Jumatano, 20/11/2019
KESHA LA ASUBUHI
Jumatano, Novemba 20, 2019
UTUKUFU WA ULIMWENGU WA ROHO
“Maana tangu zamani za kale watu hawakusikia, wala kufahamu kwa masikio, wala jicho halikuona Mungu, ila wewe, atendaye mambo kwa ajili yake amngojaye" Isaya 64:4.
📝 Wengi wamekuwa wakitamani kujipenyeza katika utukufu wa ulimwengu ujao na kuzifanya siri za milele zifunuliwe kwao, lakini huwa wanabisha hodi bure. Mambo yaliyofunuliwa ni yetu sisi na watoto wetu.... Mdhihirishaji Mkuu amefunua mambo mengi ya lazima katika akili zetu ili tuvielewe vivutio vya mbinguni na kuyathamini malipo ya ujira.
📝 Maelezo ya Yesu kuhusu mambo ya mbinguni ni namna ambayo akili ya kiroho tu inaweza kuyaelewa. Akili inaweza ikafanya kazi kwa uwezo wake wote ili kupata taswira ya utukufu wa mbinguni, lakini "jicho halikuyaona, wala sikio halikuyasikia, wala hayakuingia katika moyo wa mwanadamu, mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao" ( 1 Wakorinto 2:9 ). Viumbe wa mbinguni wenye akili wametuzunguka. ...
📝 Malaika wa nuru wanatengeneza mazingira ya kimbingu kumzunguka mtu, na kutuinua kuelekea kwenye mambo ya milele yasiyoonekana. Hatuwezi kuyaona maumbile yao kwa macho yetu ya kimwili; tunaweza kuyaona mambo ya mbinguni kwa macho ya kiroho tu. Uwezo wetu wa kibinadamu ungezimishwa na utukufu usiosemekana wa Malaika wa nuru. Sikio la kiroho peke yake linaweza kutofautisha mwafaka wa sauti za mbinguni. Kristo hana mpango wa kusisimua hisia kwa maelezo ya uangavu. ... Amejifunua kwa uwazi wa kutosha, njia, kweli , na uzima kama njia pekee ya kupatia wokovu.
📝 Hakuna jambo linalotakiwa zaidi ya hilo. Anaweza kumleta mwanadamu mpaka kwenye ukingo wa mbingu na kutuonesha kupitia katika mlango ulio wazi, utukufu wa ndani uliojaa patakatifu pa mbinguni na kung'aa kupitika katika matao yake; lakini inatupasa kuutazama kwa imani, si kwa macho ya kimwili.
Hajasahau kwamba sisi ni mawakala wa kibinadamu, kwa ajili ya kufanya matendo ya Mungu katika ulimwengu ulioharibiwa na laana. Inatupasa kutembea katika nuru ya mbinguni katika ulimwengu huu uliofunikwa na giza la kimaadili kama uvuli wa mauti, ambapo giza huifunika dunia na giza kuu kuwafunika wanadamu.
TAFAKARI NJEMA NA MUNGU AKUBARIKI
No comments
Post a Comment