Matangazo ya Kanisa Sabato ya tarehe 27 April 2019 (Mtwara SDA)


Matangazo ya Kanisa Sabato ya tarehe 27 April 2019 (Mtwara SDA)

MATANGAZO YA KANISA
Sabato ya tarehe 27/04/2019 iliyopangwa maalumu kwaajili ya kutenga tawi la Mdenga kuwa kundi imeahirishwa mpaka pale itakapo tangazwa tena.

Juma la maombi la Uwakili lililoanza tarehe 21/04/2019 litahitimishwa tarehe 27/04/2019. Mungu awabariki washiriki na waumini wote waliohudhuria.

KITABU CHA UTUME: “TUMAINI KWA FAMILIA ZA LEO” KINAPATIKANA KWA SH 1000/= TEMBELEA DUKA LA VITABU LA KANISA KWAAJILI YA KUJIPATIA NAKALA ZAKUTOSHA KUSOMA NA KUWAGAWIA WENGINE.

Kwaya ya Kanisa (Ufunuo choir) itakwenda Tandahimba kwa huduma, tuwakumbuke katika maombi.

Kikundi cha Hope Generation kitakwenda katika kanisa la K.K.K.T kwa huduma, tuwakumbuke katika maombi.

Kutakuwa na Sabato ya wageni 11/05/2019, washiriki na waumini tujiandae, pia kila mwanakikosi awasilishe mchango wake kwa mwalimu wa kikosi ili kufanikisha tukio hilo.

Kesho Jumapili tutakuwa na zoezi la usafi katika mazingira yetu ya kanisa. Waumini na washiriki wote tufike bila kukosa.

Waumini wote tunakumbushwa kuzingatia usafi wa mazingira, tutumie vyombo maalumu vya kuhifadhia taka (dustbin), tusaidiane kuwafundisha watoto matumizi ya dustbin ili kuepuka utupaji holela wa taka.

Washiriki na waumini tunakumbushwa kuchukua bahasha zetu za matoleo kwa mhazini mara baada ya kutoa Zaka na Sadaka.

Sabato ya tarehe 04/05/2019 ni sabato maalumu ya ushuhudiaji.

VIKAO NA SEMINA
Tarehe 20-27 July 2019 tutakuwa na Makambi katika mtaa wa Mtwara. Goli la sadaka ya kambi ni 8,500,000/= Goli la ubatizo kwa mwaka 2019 ni watu 124.
                
MCHANGANUO WA MCHANGO WA MAKAMBI – MATUMIZI NI KAMA IFUATAVYO
WAFANYA BIASHARA/WAFANYA KAZI 50,000/=
WATU WAZIMA 50,000/=
WANAFUNZI WA VYUO 20,000/=
WANAFUNZI SEKONDARI 10,000/=
SHULE YA MSINGI NA WATOTO 5,000/=

Mahubiri ya NET EVENT kwa njia ya Satellite yatafanyika jijini Dodoma na kurushwa na vyombo vya habari vya kanisa na mitandao ya kijamii, Kanisa la Waadventista Wasabato Mtwara litashiriki kwa kuchangia gharama za maandalizi ya mkutano 2,000,000/= pamoja na kuandaa vituo 9 vya kupokea matangazo hayo katika viunga mbalimbali vya mji wa Mtwara.
HAKIKISHA UNASHIRIKI KATIKA MBARAKA HUU KWA KUTOA SADAKA YAKO.

KUTAKUWA NA MAFUNZO YA KUFUNGA VIFAA VYA MAWASILIANO (SATTELITE DISH, STREAMING DEVICES NK) SIKU YA JUMAPILI 28/04/2019 (KESHO) KUANZIA SAA 2 ASUBUHI ILI KUSAIDIA UFANISI KATIKA VITUO VYETU, PANGA KUHUDHURIA

Kutakua na kikao cha barara la kanisa siku ya Alhamisi 02/05/2019 saa 12 jioni, wajumbe wote mnaombwa kuhudhuria.

Tuwakumbuke wagonjwa wote katika maombi, kuwatembelea na kuwasaidia.

IBADA KUU MTWARA SDA: 04 MAY 2019
MHUBIRI: FANUEL SHANGARI
MWENYEKITI: ISRAEL MGATA
FUNGU KUU/OMBI: ZAKARIA YOHANA
ZAKA/SADAKA: REBECCA MSALYA
WIMBO WA ZAKA/SADAKA: HOPE GENERATION
MHUBIRI WATOTO/WIMBO: JANETH KANGALU
WIMBO WA HUBIRI: THE HOPE GENERATION
WIMBO WA KUTOKA: TUCASA

UTARATIBU WA IBADA KATIKATI YA JUMA MTWARA SDA:

JUMATANO:
MHUBIRI: MICHAEL JOHN
MWENYEKITI: ALVANUS MKULA
KWAYA: HOPE GENERATION

KUFUNGUA SABATO:
MHUBIRI: ELIYA CHARLES
MWENYEKITI: ELLY MARIMBOCHO
KWAYA: UFUNUO

KUFUNGA SABATO:
MHUBIRI: MZEE WA ZAMU
MWENYEKITI: ERICK KAGWE
KWAYA: ZOTE

WAHUDUMU KATIKA MAKUNDI YETU:
MDENGA:
JUMATANO: ELIAS MASANO, KUFUNGUA SABATO: CHARLES MAKONGO

UTENDE:
SIKU YA SABATO MHUBIRI: ALVANUS MKULA

KITERE:
SIKU YA SABATO MHUBIRI: MICHAEL JOHN

MOMA:
MHUBIRI SIKU YA SABATO: ELLY MARIMBOCHO

MZEE WA ZAMU: VICTOR DANFORD

MASHEMASI WA ZAMU:
IFUGANIA HAULE
MWANAHAMISI SHAIBU
ESTHER GEKURA
PIUS HUNGU
TERESIA DANKAN
NEEMA DAUDI
STEVEN RUZANGI
DOTTO NGENI MIICKY

Powered by Blogger.