Siku 10 za maombi: Sherehe ya Siku ya Sabato ya Mwisho - Jumamosi (18/01/2020)
Kutafuta Roho wa Mungu
Mfumo uliopendekezwa kwa Sabato ya Mwisho
Sabato hii ya mwisho inapaswa kuwa muda wa kufurahi sana katika yale yote Mungu aliyotenda kwa ajili yako na kanisa lako kwa kipindi cha Siku hizi Kumi za Maombi. Buni siku yako kwa ajili ya kusherehekea wema wa Mungu na nguvu yake kuu. Fikiria namna ulivyopata uzoefu wa umwagwaji wa Roho Mtakatifu katika siku hizi kumi zilizopita. Sabato hii ni fursa ya kusherehekea kwa yale aliyotenda, anayotenda, na atakayotenda.
Mahitaji ya kusanyiko yanatofautiana, hivyo tafadhali fanya kazi pamoja na viongozi wa kanisa mahalia ili kueandaa mpango mahususi kwa ajili ya kanisa lako. Hapa kuna baadhi ya mambo ya kujumuisha katika ibada ya kanisa lako katika Sabato ya Mwisho.
Mapendekezo ya Ratiba ya Ibada
Programu za nyongeza kama utapenda

- 04:30 Nyimbo za kusanyiko.
- 04:45 Ukaribisho, matangazo, na maelezo ya matukio.
- 05:00 Wimbo wa Sifa (mapendekezo: “Mungu Atukuzwe #3”). Watu wasimame. 05:05 Usomaji kwa kuitikia. Watu wasimame.
- 05:10 Maombi ya kusanyiko. Yakiongozwa na mchungaji au mzee wa kanisa. Hili ni ombi la sifa, si kwa ajili ya mahitaji au ombi la kusihi. Watu wapige magoti.
- 05:15 Maombi ya kuungama. Watu wakidumu kupiga magoti. Kusanyiko liombe kwa ukimya, kisha kiongozi wa maombi amshukuru Mungu kwa kusikia maombi yetu na kutusamehe dhambi zetu kulingana na 1 Yohana 1:9. Baada ya maombi, watu wanaweza kuketi.
- 05:20 Wito na ukusanyaji wa matoleo, ikifuatiwa na ombi la kumshukuru Mungu kwa mahitaji anayotupatia na kumuomba abariki zaka na sadaka hizo.
- 05:25 Wimbo maalumu. Chagua wimbo unaoendana na wazo kuu la maombi. 05:30 Mchungaji au kiongozi mwingine atoe ujumbe mfupi kuhusu umuhimu wa maombi katika maisha yetu.
- 05:40 Mchungaji au kiongozi mwingine aite watu wasogee mbele ikiwa wana maombi ya mizigo maalumu. Toa muda kwa ajili ya watu kushiriki ikiwa watapenda. Kisha mtu aongoze ombi la kusihi, akiwasilisha maombi kwa Mungu. Watu wanaweza kurudi na kuketi baada ya hapo.
- 05:55 Maombi kwa ajili ya huduma mahususi. Mfano: maombi kwa ajili ya jamii, kwa ajili ya watu wanaomhitaji Yesu, kwa ajili ya shule mahalia ya Kikristo na huduma za vijana, kwa ajili ya konferensi na kanisa la kiulimwengu, kwa ajili ya ndoa na familia. Kila kipengele kinaweza kuongozwa na mtu anayehusika na huduma husika; mfano, mwanafunzi anaweza kuombea shule.
- 06:10 Wimbo wa kufunga wa kuweka wakfu (Mapendekezo: “Uniongoze Yehova #156; Huniongoza Mwokozi #151”).
- 06:15 Maombi na mibaraka ya mwisho.
Programu za nyongeza kama utapenda
- Shuhuda kwa maombi yaliyojibiwa
- Muda wa maombi ya makundi madogo
- Matangazo ya shughuli za maombi zijazo
- Visa vya watoto kuhusu maombi
- Vipindi vinavyowasilishwa na vijana
No comments
Post a Comment