VIJANA MTWARA SDA WAAZIMIA KUNUNUA VYOMBO VYA KISASA!!!
Katika hali ya kutia moyo, vijana wa kanisa la Waadventista Wasabato Mtwara mjini wameamua kuungana ili kuanza mchakato wa ununuzi wa vyombo vya kanisa vitakavyo tumika katika ibada kanisani hapo. Wakizungumza katika kikao chakwanza kilicho fanyika Sabato ya tarehe 27/12/2014 baada ya ibada, vijana hao wamekubaliana kutekeleza adhma hii kwa awamu. Ili kurahisisha shughuli hii vijana wamegawanyika katika makundi matatu ambayo ni;
1. Vijana wenye ajira, Wafanya biashara na Waliopo masomoni huku wakifanya kazi
2. Vijana waliopo katika vyuo
3. Vijana waliopo sekondari.
Katika lila kundi kuna viongozi watakaokuwa wakileta mrejesho wa maendeleo.
Bwana awabariki kwa njozi hii nzuri.

No comments
Post a Comment