SABATO YA TAR 23 JULY, 2016 - SEMINA YA AMR - MTWARA SDA

Sabato ya Tarehe 23 July 2016 imekuwa sabato yapekee na yakupendeza ambapo semina ya AMR iliendeshwa katika kanisa la Waadventista Wasabato - Mtwara. Semina hio iliyoendeshwa na Mchungaji Dominick Mapima ilielekeza mbinu za kupeleka habari njema kwa ndugu zetu waislam.
Ikumbukwe kuwa mkoa wa Mtwara ni miongoni mwa mikoa ambayo dini ya kiislamu imeenea sana.
Kabla ya semina hiyo, mchungaji wa mtaa wa mtwara Pr Sospeter alifungua kipindi na kumkaribisha mchungaji Zetti Ndola kutoka makao makuu ya Union ya Kusini mwa tanzania (SEC) ambaye alieleza mikakati mbalimbali ya Union katika mikoa ya kusini na baada ya kuhitimisha ndipo mchungaji Mapima akasimama na kuanza semina iliyokuwa na mvuto wa pekee.
Shuhudia picha za matukio mbalimbali
KWAYA YA UFUNUO + MCHUNGAJI MAPIMA WAKIIMBA WIMBO WA BIBLIA NI TAA





MCHUNGAJI NDOLA AKIFAFANUA MIKAKATI YA UNION YA KUSINI


WASHIRIKI WAKIIMBA WIMBO WA BIBLIA NI TAA


MCHUNGAJI ZETTI NDOLA AKIWA NA BIBLIA YAKE HUKU AKIIMBA WIMBO WA BIBLIA NI TAA

No comments

Powered by Blogger.