MATANGAZO YA KANISA, SABATO YA TAREHE 28/09/2019

MATANGAZO YA KANISA, SABATO YA TAREHE 28/09/2019
Karibu katika blog ya Kanisa la Waadventista Wasabato - Mtwara, Yafuatayo ni matangazo ya kanisa Sabato ya tarehe 28/09/2019.


  1. Leo ni Sabato maalumu, kutakuwa na huduma ya Meza ya Bwana, pia tutakuwa na huduma ya Ubatizo.
  2. Keso Jumapili, mashemasi wote wafike kanisani kwaajili ya usafi wa vifaa vitakavyotumika katika meza ya Bwana na Ubatizo.
  3. Waimbaji wa Hope Generation, Kwaya ya Ufunuo wakumbuke kufunga viti na kufunga milango ya kanisa mara baada ya mazoezi, pia wale wote wanaofanya vikao mbalimbali kanisani wanakumbushwa kufunga viti mara baada ya vikao.
  4. Leo, mahubiri kwa njia ya Sattelite yataanza kurushwa kutoka katika kanisa la Ikulu jijini Mbeya. Tutakuwa na kituo hapa kanisani hivyo waalike ndugu jamaa na marafiki kushiriki, wajulishe wasioweza kufika kuwa mahubiri yatarushwa na vyombo vya habari vya Star TV na Star Religion hivyo wayafuatilie popote watakapokuwa.
  5. Sabato ya tarehe 5 October, 2019 tutakuwa na ugeni wa kwaya ya kanisa la KKKT Mtwara ambao watakuja kushiriki nasi katika huduma ya uimbaji.
  6. Sabato ya 5 October, 2019 ni sabato yakwanza ya robo hivyo itakuwa ni siku ya kufunga na kuomba.
VIKAO, SEMINA NA MIKUTANO
  1. Kesho Jumapili 29 September, 2019 kutakuwa na kikao cha baraza la huduma kuanzia saa 2 asubuhi. Wajumbe wote wazingatie muda.
  2. Kutakuwa na kongamano la mwaka la wana taaluma na wajasiriamali litakalofanyika NSSF ilala jijini Dar -es- Salaam kuanzia tarehe 11 mpaka 14 October, 2019. Kiingilio ni 100,000/= ikijumuisha mlo wa mchana, makabrasha na viburudisho.
UHAMISHO WA USHIRIKA
Cecilia Yobu Massawe kutoka kanisa la Waadventista Wasabato Hai - Kilimanjaro kuja Mtwara SDA (Linasomwa kwa mara ya pili)
MATANGAZO YA NDOA
  1. Tunatangaza kusudio la kufunga ndoa takatifu kwa mara ya nne kati ya ndugu Daniel Petro Ntogwalama na Leah Thobias Mwinuka; Itakayofungwa Jumapili ya tarehe 29 September, 2019 katika kanisa la Waadventista Wasabato Kisiwani - Iringa.
  2. Tunatangaza kusudio la kufunga ndoa takatifu kwa mara ya tatu kati ya ndugu Juma John Elisha na Neema Raphael Darmian; Itakayofungwa Jumapili ya tarehe 06 October, 2019 hapa Mtwara SDA.
WAGONJWA
Tuendelee kuwaombea wagonjwa wote na kuwatembelea kwaajili ya faraja.

UTARATIBU WA IBADA KATIKATI YA JUMA
JUMATANO: 
MHUDUMU: DAVID P. JOSHUA
MWENYEKITI: SARAH SAMWEL
KWAYA: ZOTE

IJUMAA (KUFUNGUA SABATO):
MHUDUMU: YOHANA RAPHAEL
MWENYEKITI: PHIBE WILFRED
KWAYA: ZOTE

UTARATIBU WA IBADA KUU SABATO IJAYO MAKUNDINI NA KWENYE MATAWI YA SHULE YA SABATO
MDENGA: MICHAEL JOHN
NALIENDELE: AMOS KAMANDO
KING DAVID: ERICK JULIUS
MTWARA GIRLS: JANETH KANGALU
KITERE: ELLY MARIMBOCHO
MOMA: ELIAS MASSANO
IBADA KUU MTWARA SDA
MHUBIRI: ALIYEPEWA TAARIFA YA KUHUDUMU
MWENYEKITI: ISRAEL MGATA
FUNGU KUU/OMBI: IFUGANIE HAULE
ZAKA/SADAKA: EDWARD KISHIWA
WIMBO WA ZAKA NA SADAKA: HOPE GENERATION
MHUBIRI WA WATOTO: ELIFURAHA ANDREW
WIMBO WA HUBIRI: KWAYA YA UFUNUO
WIMBO WA KUTOKA: KWAYA YA UFUNUO
MASHEMASI WA ZAMU
  1. DAVID P. JOSHUA (SHEMASI MKUU)
  2. BENINO NGESA (ATAKUSANYA SADAKA)
  3. GLORY MPILI (ATAKUSANYA SADAKA)
  4. JENIPHER MSALYA
  5. YOHANA RAPHAEL
  6. BARAKA ODONGO
  7. DIANA MICHAEL
MUNGU AKUBARIKI
Powered by Blogger.