Siku 10 za maombi: Siku ya Kumi - Ijumaa - (17/01/2020)
Kudumu katika Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele… Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu… Mtu akinipenda, atalishika neno langu; na Baba yangu atampenda; nasi tutakuja kwake, na kufanya makao kwake.” Yohana 14:16, 18, 23.
Ushuhuda
“Unapoamka asubuhi, huwa unahisi hali yako ya kukosa msaada, na hitaji lako la nguvu kutoka kwa Mungu? Na huwa unaeleza mahitaji yako kwa unyenyekevu, na kwa moyo kwa Baba yako wa Mbinguni? Kama ndivyo, malaika huweka alama maombiyako, na ikiwa maombi haya hayakutoka kwenye midogo isiyo kusudia, unapokuwa katika hatari ya kutenda kinyume bila kutambua, na kuweka mvuto utakaowaongoza wengine kutenda kinyume, malaika wako wa ulinzi atakuwa kando yako, akikusihi kuwa bora Zaidi, akikuchagulia maneno, na kutia mvuto katika matendo yako” (Ellen White, Messages to Young People, uk. 90).
Sabato moja, nilikuwa nimesimama sehemu ya kuoshea vyombo katika ukumbi wa mikutano yetu ya ushirika nikiwa naosha vyombo baada ya kutumia vyakula tulivyobeba. Mwanafunzi mdogo kutoka Urusi alikuwa akikausha vyombo. Nilifahamu hakuwa Mkristo, hivyo niliomba kwa ukimya kuhusu namna ninavyoweza kutumia muda huu tunaoosha vyombo pamoja. “Nina swali kwako, ikiwa hutojali,” nilisema. “Sawa, ni nini?” alijibu. “Ni kwa nini watu wengi Urusi si Wakristo?” niliuliza. “Unaweza pia kuniuliza kwa nini mimi si Mkristo,” alisema akiwa na tabasamu dogo. “Sawa,” nilisema kwa sauti ya upole, “ni kwa nini wewe si Mkristo?” “Sina tu uthibitisho wa uwepo wa Mungu,” alisema. Kasha aliuliza, “Kwa nini wewe ni Mkristo?” “Kwa sababu nina ushahidi wa kutosha!” nilijibu. Alicheka na kusema, “Sawa, ushahidi wako ni upi?” Kisha nilimpatia ushuhuda wangu wa yale Mungu aliyonitendea.
“Nina uchunguzi, ikiwa utapenda kujaribu,” nilisema. “Ninaamini ukifanya uchunguzi huu utapata ushahidi wa Mungu. Ningependa utumia muda mchache kwa siku 30 zinazofuat kusoma kutoka kwenye kitabu cha Yohana. Ukimaliza kabla siku 30 hazijaisha, anza tena. Pia ningependa uomba Mungu wakati mtu mwingine ye yote hafahamu. Zungumza naye kuhusu mambo ambayo wewe pekee ndiye unayafahamu, na muombe kitu ambacho wewe pekee ndiye unafahamu, kasha uone kitakachotokea.” “Sawa,” alisema, “hilo linaonekana jambo rahisi sana. Utakua uzoefu wa kuvutia.”
Kama mwanafunzi wa kubadilisha mazingira alipaswa kwenda po pote familia yake iliyompokea itakapokwenda ili aweze kuonja ladha ya tamaduni. Hivyo, kila juma alihudhuria kanisani kwa sababu hilo ndilo familia iliyomhifadhi kwa muda ilitenda. Majuma mawili baada ya kuanza utafiti huo, nilihudhuria kanisani kwake na kumuuliza, “Unaendeleaje na utafiti?” Alikuwa makini lakini mwenye kufurhi na alisema, “Sielewi kinachotokea. Bado nina juma moja, lakini sina uhakika kwamba naweza tena kusema hakuna Mungu.” “Hilo ni jambo jema kwako,” nilijibu. “Endelea.
Nina uhakika utapata ushahidi ziadi wa Mungu ikiwa utafungua akili yako.” Alitabasamu na kunishukuru alipoondoka siku ile. Alirudi kwao Urusi kabla ya siku 30 kuisha, lakini ninafahamu alikua akiunganika Zaidi na Mungu!
Ni kwa namna gani tunadumu katika uwepo wa Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu?
1. Kwa kutumia muda katika kujifunza Biblia kwa moyo na akili zilizo wazi. Yesu ndiye Neno (Yohana 1:14; 14:6-9), na ikiwa tumemuona, tumemuona Baba. Pia, Roho Mtakatifu ndiye alivuvia Neno la Mung (2 Petro 1:21). Hivyo, kadri tunavyosoma Biblia na kuamini mafundisho na ahadi zake, tunabadilishwa na kuwa katika mfano wa Kristo (2 Wakorintho 3:18).
2. Pili, tunapoomba kwa Mungu, tukifungua mioyo yetu kwake kama tufanyavyo kwa Rafiki, Roho Mtakatifu husogea karibu, mioyo yetu hulainishwa, na tunaweza kushinda majaribu yake kwa nguvu za Mungu.
3. Mwisho, tunapotii Biblia na kushiriki na wengine, tunavutwa karibu na moyo wa Mungu, na utu wetu wa ndani huwa na Amani (Mathayo 11:28-30).
Mafungu ya Biblia ya Kuombea
Mapendekezo ya Maombi
Nyimbo Zinazopendekezwa

- 2 Petro 1:21 – Roho Mtakatifu alivuvia Biblia. Tunapoisoma na kuikubali, tunadumu katika uwepo wake na wa Yesu na wa Baba (Yohana 14:23).
- Luka 11:11-13 – Tunapoomba uwepo wa Mungu tunazidsha nguvu ya Roho Mtakatifu ndani yetu na kutuzunguka.
- Matendo 2:1-4 – Roho Mtakatifu anatutaka tushiriki kile alichotufundisha Mungu na namna alivyotubariki. Anataka watu wote kila mahali waokolewe.
- 1 Timotheo 2:1-4 – Tunapoomba, Roho Mtakatifu hubariki dunia kutuzunguka na huwaongoza watu katika wokovu.
- Matendo 5:31, 32 – Tunapotii kile alichotuambia tutende, tunaongeza uwepo wa Rooho Mtakatifu na mibaraka katika maisha yetu.
- Warumi 8:26 – Roho Mtakatifu anataka kutusaidia kuwa watu wa maombi. Hakika mibaraka itafuata (2 Nyakati 7:14).
Mapendekezo ya Maombi
- Mpendwa Baba wa mbinguni, nipatie njaa ya neon lako ili nifurahie kutumia muda pamoja nawe. Ninaposoma Biblia, nipatie uelewa wa wazi wa tabia yako na nia yako katika maisha yangu.
- Yesu, tafadhali tuma Roho Mtakatifu katika maisha yangu na nifanye kuwa mtu wa maombi. Nibadilishe na kuwa mwanamaombi mwenye nguvu ili wengi waweze kuokolewa na kuwekwa huru kutoka kwenye vifungo vya giza ya Shetani.
- Naomba akili na moyo wangu viwe makini kwa nia yako. Nifanye nitembee katika utii kamili wa amri zako na Neno lako lote.
- “Nipokee, Ee Bwana, kwa utakatifu wako, ninaweka mipango yangu yote miguuni pako. Nitumie leo katika huduma yako. Kaa pamoja name, na ruhusu kazi zangu zote kujengwa kwako” (Ellen White, Steps to Christ, uk. 70).
- Bwana, tunawainua viongozi wetu wa kanisa duniani. Tafadhali wapatie hekima kadri wanavyofanya maamuzi na kuwaongoza watu wako.
- Tunaomba kwa ajili ya watoto wetu. Tafadhali watie nguvu ili wasimame imara kwa ajili yako wanapokutana na vikwazo na misukumo. Wasaidie kufanya chaguzi sahihi na kusimamia ukweli.
- Tunaomba kwa ajili ya familia ambazo mazingira yao yamejazwa vurugu, huzuni, na kuchanganyikiwa.
- Bwana, tunaomba uamsho mkuu wa utakatifu usafishe kanisa lako katika siku za mwisho. Tunaomba tusimamie ukweli hata mbingu zikianguka.
- Tunaomba kwa ajili ya majina saba katika orodha zetu. Tafadhali muonyeshe kila mmoja namna Yesu anavyompenda.
- Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa
- Karibu na Wewe Mungu Wangu #152
- Univute Karibu Baba #148
- Asubuhi #89
- Tumesikia Mbiu #108
No comments
Post a Comment