Siku 10 za maombi: Siku ya Tisa - Alhamisi - (16/01/2020)
Kazi ya Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Baada ya hayo naliona malaika mwingine, akishuka kutoka mbinguni, mwenye mamlaka kuu; na nchi ikaangazwa kwa utukufu wake… Kisha nikasikia sauti nyingine kutoka mbinguni, ikisema, Tokeni kwake, enyi watu wangu, msishiriki dhambi zake, wala msipokee mapigo yake.” Ufunuo 18:1, 4.
Ushuhuda
“Huduma ya Roho Mtakatifu ya kutenda kazi ndani yetu ndilo hitaji letu kuu. Roho ni mtakatifu katika kazi na udhihirisho wake. Mungu anataka uwe na ujazo wa kiroho; ndipo utafanya kazi kwa nguvu ambayo hukuwahi kuifahamu hapo kabla. Upendo na Imani na tumaini vitadumu. Unaweza kuendelea katika Imani, ukiamini kwamba Roho Mtakatifu yupo pamoja nawe” (Ellen White, Evangelism, uk. 299).
Siku moja kutatokea uamsho mkubwa kati ya watu wa Mungu walio wa kweli duniani. Roho Mtakatifu atashuka kwa nguvu kuu. Ushukaji huu wa Roho Mtakatifu ulifananishwa na mvua ya masika katika nyakati za Biblia, ambayo ingenyesha katika Mashariki ya Kati, ikikomaza mazao na kuandaa mavuno (Zakaria 10:1). Siku moja watu wa Mungu watatoka na kushiriki Imani yao kwa njia yo yote ile iwezekanayo. Miujiza itatendeka kupitia kwa Kristo. Maelfu, pengine mamilioni, wataokolewa. Kazi ya Roho Mtakatifu ni kuokoa waliopotea, na hakuna furaha kuu zaidi kuliko kushiriki katika kazi hiyo.
Katika Sabato moja, Lance na mke wake, Ranea, walikuja katika kanisa letu la Waadventista wa Sabato. Kuna mtu aliacha kitabu kiitwacho Bible Readings for the Home (Masomo ya Biblia kwa ajili ya nyumbani) mlangoni mwa nyumba yao. Kwa sababu ya hali fulani katika maisha yao, Lance na Renae waliamua kuangalie kile kitabu kilisema nini. Wakikiangalia kitabu, waligundua mada ya Sabato, ambayo kwa hakika ilivuta hamasa yao.
Walijifunza kwa kina kipande hivyo na walidhihirishiwa kwamba walihitaji kutafuta kanisa lililochapisha kitabu hicho. Baada ya kugundua kwamba kilichapishwa na Waadventista wa Sabato, walitafuta kanisa letu na kuhudhuria Sabato iliyofuata. Lance alishikilia kitabu hicho na kuuliza, “Je, kanisa lako linachapisha kitabu hiki?” “Ndiyo, tunafanya hivyo!” nilijibu. “Vema,” Lance aliendelea, “Tuna maswali mengi. Kuna uwezekano wa wewe kuja nyumbani kwetu kutupatia mafundisho ya Biblia?” Hakika, niliwahakikishia kwamba ningefurahi kufanya hivyo.
Nilipowatembelea, niligundua kwaba Lane na Renae na vijana wao wa kiume wwili walitamani mabadiliko makubwa katika maisha yao. Walikuwa ni wahanga wa pombe na mambo ya kuharibu, na ndoa yao ilikuwa ikiteseka sana. Nilifahamu kwamba walihitaji nguvu ya Yesu. Kadri niliposhiriki injili, huku nikidumu msaada wa Mungu moyoni mwangu, niliweza kuona Roho Mtakatifu alikuwa akinena nao ndani sana. Nilimaliza uwasilishaji wa injili na kuuliza, “Je, kuna sababu yo yote ya kuwafanya msitoe maisha yenu kwa Yesu?” Walijibu kwamba wangefurahia msamaha na wokovu wa Yesu. Saa ile ile tulipiga magoti na kuomba, na niliwaongoza katika ombi la kuungama na kumkubali Yesu kama Bwana na Mwokozi. Huku wakitokwa machozi walirudia ombi lililosema, na tuliinuka magotini tukiwa na furaha. Nguvu ya muujiza ya Roho Mtakatifu ilikuwa dhahiri. Sasa walizaliwa kama watoto wa Mungu.
Nilipowasili kwa ajili ya kipindi chetu kilichofuata kwa juma, kabla sijamaliza hatua tatu kuelekea sebuleni, Lance aliuliza, “Mchungaji, unafikiri nini juu ya uvutaji wa sigara? Unafikiri ni jambo Mkristo anapaswa kufanya?” Nilipendekeza tujifunze mada ya maisha yenye afya usiku ule, ambayo tulijifunza. Kama matokeo ya kipindi kile ha kujifunza Biblia na siku zilizofuata za mimi kuwatembelea, Lance na Renae walikuwa huru kutoka kwenye vifungo vyote ambavyo Shetani aliwafunga navyo. Na karibuni walibatizwa na wote wakawa wasaidizi wenye nguvu katika shauri la Kristo, wakishiriki shuhuda zao na kutoa masomo ya Biblia kwa wanafamilia na marafiki. Wao pia walianza kushiriki katika kazi ya Roho Mtakatifu kwa kusambaza injili kwa wote waliowazunguka. Ni muujiza wa ajabu kiasi gani!
Mafungu ya Biblia ya Kuombea
Mapendekezo ya Maombi
Nyimbo Zinazopendekezwa
Nipo Bwana Nitume #107
Sauti Yake Mchungaji #193
Nasikia Sauti Yako #142

- Mathayo 28:19, 20 – Kila mfuasi wa Kristo anapaswa kutenda awezalo kutenda ili kusambaza injili ya wokovu.
- Yohana 16:13 – Roho Mtakatifu anapotenda kazi, watu watavutwa katika kweli ya Neno la Mungu.
- Matendo 4:29-31 – Kanisa la awali lilimuomba Mungu awajaze kwa Roho Mtakatifu ili waweze kutangaza Neno la Mungu kwa ujasiri.
- Waefeso 4:11, 12 – Karama za Roho Mtakatifu ni kwa ajili ya kuwaandaa Wakristo kwa ajili ya kazi ya utume na kulijenga kanisa la Mungu.
- Matendo 9:36-42 – Kusudi la miujiza ni kwamba watu wawe na ushahidi unaoweza kuwafanya wamuamini Yesu.
- Marko 16:15-18 – Enendeni ulimwenguni, ponyeni wagonjwa, hubirini injili, dhihirisheni tabia ya Mungu kwa kila mtu.
- Isaya 6:8 – Mimi hapa, Bwana. Nitume mimi.
Mapendekezo ya Maombi
- Mpendwa Baba wa mbinguni, nifanye kuwa mtumishi wako na nisaidie kushiriki ujumbe wa upendo na wokovu wako.
- Kwa neema yako, Bwana, ninajitoa kufundishwa na kuandaliwa kushiriki injili kwa namna utakayonichagulia.
- Nibatize kwa Roho wako Mtakatifu ili niongozwe kutoka ndani kuweza kushinda vikwazo na hofu. Nifanye niwe mfereji wa nguvu yako na ujumbe unaookoa wa Kristo aliyesulubishwa na kufufuka.
- Bariki jitihada za wachungaji, watendakazi wa Biblia, waalimu, na wainjilisti ulimwenguni. Wajaze kwa nguvu kuu na mamlaka. Tunaomba mamilioni ya watoto wako waokolewe kila mwaka!
- Tafadhali ruhusu familia zetu kudhihirisha upendo wako katika nyumba zetu na jamii zetu. Tunakuomba ulete uelewano katika familia, ponya mahusiano yaliyovunjika, linda wenye hatari ya kukumbwa na unyanyasaji, na dhihirisha nguvu yako ya kutakaso katika hali zinazoonekana kutokuwa na tumaini.
- Tunaomba washiriki wa kanisa letu, wachungaji, na viongozi duniani wajilishe kwa Neno la Mungu kila siku. Tuweze pia kukutafuta kila siku katika maombi binafsi. Tukumbushe kwamba bila wewe, hatuwezi fanya lo lote.
- Tunakuomba uinue wauguzi na madaktari ili kuanzisha makanisa kati ya makundi 1,978 ya watu katika nchi 22 za Divisheni ya Afrika Magharibi na Kati.
- Tunaomba kwa ajili ya watu milioni 49 katika miji 19 ambayo haijafikiwa Zaidi ya Divisheni ya Tran-Europe
- Bwana, tafadhali saidia vijana wetu wasihubiri tu lakini pia waishi hubiri hilo. Tunamba Mungu abariki jitihada za Siku ya Vijana Ulimwenguni (Global Youth Day) na mikakati 100,000 ya uhusishwaji wa kila mshiriki (TMI)
- Tunaombea watu saba katika orodha zetu za maombi. Wapatie mioyo ya kukufahamu kama Neno lako linavyosema katika Yeremia 24:7.
- Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa
Nipo Bwana Nitume #107
Sauti Yake Mchungaji #193
Nasikia Sauti Yako #142
No comments
Post a Comment