Siku 10 za Maombi: Siku ya Kwanza - Jumatano - (08/01/2020)
Siku ya Kwanza - Jumatano - (08/01/2020)
Hitaji Letu la Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Matendo 1:8
Ushuhuda
“Ikiwa hii ndiyo njia tunayoweza kutumia kupata nguvu, kwa nini hatuoni njaa na kiu ya zawadi ya Roho? Kwa nini hatuizungumzii, hatuiombei, na hatuhubiri kuhusu zawadi hiyo? Bwana yu tayari zaidi kumtoa Roho Mtakatifu kwa wale wanaomtukimikia kuliko ilivyo kwa wazazi kutoa zawadi nzuri kwa watoto wao. Ili kupata ubatizo wa Roho kila siku, kila mtumishi anapaswa kuwasilisha ombi lake kwa Mungu” (Ellen White, The Acts of the Apostles, uk. 50).
Kabla tu ya kuhitimu chuo nikiwa na shahada ya theolojia, nilisoma kitabu kinaitwa They Found the Secret (Wameipata Siri) kilichoandikwa na V. Raymond Edman. Kitabu hiki hutueleza kuhusu wanaume na wanawake 20 waliofikia kipindi cha hatari ya kiroho katika maisha yao kilichopelekea uzoefu wa badiliko thabiti. Kitendo hiki kilifuatiwa na umwagwaji wa Roho Mtakatifu katika maisha yao. Wakawa watu waliobadilika na kuwa wapya – na kuongoza mamilioni kwa Kristo – kwa sababu walijazwa kwa Roho Mtakatifu. Ninapofikiria maisha yangu kama mume, baba mpya, na mchungaji mtarajiwa, niliandika dondoo katika kitabu hicho: “Ninamhitaji Roho Mtakatifu pia.”
Tangu hapo nimefanya kipaumbele changu cha kwanza kuwa ni kudumisha uzoefu wangu wa badiliko na kutafuta ubatizo wa kibiblia wa Roho Mtakatifu kupitia kujifunza Biblia, utii, kushiriki na wengine, na maombi. Katika mwaka wangu wa kwanza wa uchungaji, niliitwa kumtembelea mhazini wa kanisa letu, aliyegunduliwa kuwa na kansa. Tuliomba na kumpaka mafuta kama Biblia inavyosema tufanye. Baada ya siku kadhaa, alishiriki kwa furaha kwamba aliponywa kabisa kansa yake! Ndipo nilifahamu kuwa Mungu alikuwa akisikia maombi yangu na kwamba alikubali jitihada zangu za kuyaishi maisha yangu kwa ajili yake. Vipi kuhusu wewe? Je, unamhitaji Roho Mtakatifu katika maisha yako?Hitaji Letu la Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Lakini mtapokea nguvu, akiisha kuwajilia juu yenu Roho Mtakatifu; nanyi mtakuwa mashahidi wangu katika Yerusalemu, na katika Uyahudi wote, na Samaria, na hata mwisho wa nchi.” Matendo 1:8
Ushuhuda
“Ikiwa hii ndiyo njia tunayoweza kutumia kupata nguvu, kwa nini hatuoni njaa na kiu ya zawadi ya Roho? Kwa nini hatuizungumzii, hatuiombei, na hatuhubiri kuhusu zawadi hiyo? Bwana yu tayari zaidi kumtoa Roho Mtakatifu kwa wale wanaomtukimikia kuliko ilivyo kwa wazazi kutoa zawadi nzuri kwa watoto wao. Ili kupata ubatizo wa Roho kila siku, kila mtumishi anapaswa kuwasilisha ombi lake kwa Mungu” (Ellen White, The Acts of the Apostles, uk. 50).
Kabla tu ya kuhitimu chuo nikiwa na shahada ya theolojia, nilisoma kitabu kinaitwa They Found the Secret (Wameipata Siri) kilichoandikwa na V. Raymond Edman. Kitabu hiki hutueleza kuhusu wanaume na wanawake 20 waliofikia kipindi cha hatari ya kiroho katika maisha yao kilichopelekea uzoefu wa badiliko thabiti. Kitendo hiki kilifuatiwa na umwagwaji wa Roho Mtakatifu katika maisha yao. Wakawa watu waliobadilika na kuwa wapya – na kuongoza mamilioni kwa Kristo – kwa sababu walijazwa kwa Roho Mtakatifu. Ninapofikiria maisha yangu kama mume, baba mpya, na mchungaji mtarajiwa, niliandika dondoo katika kitabu hicho: “Ninamhitaji Roho Mtakatifu pia.”
Mafungu ya Biblia ya Kuombea
Siku moja Paulo aliuliza watu 12 kutoka Efeso, “Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” (Matendo 19:2). Je, wewe ungejibu vipi? Wale Waefeso walisema, “La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.”
- Warumi 8:16 – Roho Mtakatifu atapokuja kati yetu, tutaungama dhambi zetu na kupokea zawadi ya wokovu kupitia kwa Yesu. Tutakuwa na uhakika wa wokovu kwa sababu sisi ni watoto wa Mungu.
- Ezekieli 36:25-27 – Uwepo wa Roho Mtakatifu utatupatia akili mpya na moyo mpya. Tutakuwa na ushindi dhidi ya dhambi zetu na kuona ukuaji halisi wa tabia.
- Yohana 7:38, 39 na Wagalatia 5:22, 23 – Tunapojazwa kwa Roho Mtakatifu, tunda la Roho – tabia ya Mungu – itatiririka kutoka kwetu kama mito ya maji ya uzima.
- Matendo 4:13, 31 – Uwepo wa kudumu wa Roho Mtakatifu utatuhamasisha na kututia nguvu kushiriki injili na watu wengi kadri iwezekanavyo.
- Yohana 16:13 – Kadri Roho anavyoishi ndani yetu, tutakuwa na njaa na upendo kwa Biblia, na atatuongoza katika kweli yote. Kweli hii si uelewa tu wa mambo lakini tabia halisi ya Kristo, ambaye ndiye kweli.
- Warumi 8:26, 27 – Kadri tunavyoomba katika Roho Mtakatifu, tutakuwa na nguvu katika maombi yetu na tutaona majibu mengi ya miujiza kwa maombi yetu.
Yesu alisema kwamba kutakuwa na makundi mawili ya Wakristo kabla tu ya kurudi kwake (Mathayo 25). “Ndipo ufalme wa mbinguni utakapofanana na wanawali kumi, waliotwaa taa zao, wakatoka kwenda kumlaki bwana arusi” (Mathayo 25:1). Wanawali watano walikuwa wapumbavu na hawakuwa na mafuta (uwepo wa Roho Mtakatifu; tazama Zakaria 4:1-6) katika akiba. Hawa huwakilisha wale wanaoonekana kumfuata Yesu lakini hawatendi hivyo. Wana dini bali si wa kiroho. Hivyo Yesu aliwaambia, “Siwajui ninyi!” Wanawali watano werevu walikuwa na mafuta ya kutosha. Walijazwa kwa Roho Mtakatifu na walikuwa na uhusiano halisi na Yesu.
Baada ya kupaa kwa Kristo, kama utii kwa agizo lake, wanafunzi wake walibaki Yerusalemu. “Nao walikuwa daima ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu” (Luka 24:53). Wakati ambao hawakuwepo hekaluni, walikuwa katika chumba cha juu. “Hawa wote walikuwa wakidumu kwa moyo mmoja katika kusali, pamoja nao wanawake, na Mariamu mama yake Yesu, na ndugu zake” (Matend 1:14). Siku kumi baadae wote walibatizwa katika nguvu ya Roho Mtakatifu (Matendo 2), na watu 3,000 walibadilishwa ndani ya siku moja katiku sehemu ile moja!
Mapendekezo ya Maombi

- Tunakuja katika uwepo wako tukiwa na shukrani, na tunaingia katika nyumba yako tukiwa na sifa. Hatuna maneno yanayoweza kueleza kwa ufasaha namna tunavyokushukuru wewe na yale uliyotutendea. Kwa furaha na unyenyekevu tunaongeza sifa zetu za kibinadamu kwa zile sifa za malaika wasio na dhambi, ambao hufurahia daima kukuabudu!
- Tafadhali badilisha moyo wangu, Ee Mungu, uufanye mpya daima. Nisasishe kutoka kwenye dhambi na niandae kumpokea Roho Wako (Zaburi 51:7, 10).
- Bwana, tafadhali tuma uamsho wa kweli kati ya watu wako, wanaotambulika kwa tunda la Roho Mtakatifu (Wagalatia 5: 22, 23).
- Tubatize kwa Roho Mtakatifu na tupatie nguvu ya kutangaza injili kwa dunia iliyopotea katika giza (Matendo 1:5-8).
- Ee Bwana, naomba urehemu familia yangu, marafiki, wafanyakazi, na wanafunzi wenzangu. Waokowe, na naomba niwe msaidizi wako upande huu (Mathayo 28:19, 20).
- Wabariki wachungaji, waalimu, wainjilisti, watendakazi wa Biblia, na watendakazi wa kanisa letu kwa nguvu ya Roho Mtakatifu (1 Timotheo 2:1-4).
- Ee Bwana, tafadhali warehemu walionyanyaswa na kuteswa na wapatie ulinzi wako na ukombozi kutoka kwa mikono ya wale wanaotafuta kuwaumiza (Zaburi 91).
- Tafadhali bariki mamia ya maelfu ya shughuli za kuwafikia watu ulimwenguni kwa mwaka 2020. Tunaomba hasa kwa ajili ya efoti za uinjilisti za Uhusishwaji wa Kila Mshiriki huko Papua New Guinea mwezi Mei 2020.
- Tunaomba kwa ajili ya uamsho wa kiroho kati ya vijana Waadventista wa Sabato wanaohudhuria vyuo vya kiserikali ulimwenguni. Hebu na wawe mabalozi mashuhuri wa Kristo.
- Tunaomba kwa ajili ya asilimia 69 ya idadi ya watu duniani ambao hawajapokea habari zisizo na mawaa za Yesu.
- Tunaomba kwa ajili ya watu milioni 62 katika miji 28 ambayo haijafikiwa Zaidi katika unioni ya zamani ya Kirusi (Divisheni ya Ulaya na Asia).
Nyimbo Zinazopendekezwa
- Nijaze Sasa #40,
- Moyo Safi #116
- Nakupenda Zaidi #48
No comments
Post a Comment