Siku 10 za maombi: Siku ya Pili - Alhamisi- (09/01/2020)
Ushuhuda wa Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.” Yohana 16:8
Ushuhuda
“Roho Mtakatifu ni nafsi, kwani hushudia pamoja na nafsi zetu kwamba sisi ni watoto wa Mungu. Ushuhuda huu unaposhuhudiwa, hubeba pamoja nao uthibitisho wake. Katika nyakati kama hizi tunaamini na kuwa na uhakika kwamba sisi ni watoto wa Mungu” (Ellen White, Evangelism, uk. 616).
Roho Mtakatifu hutenda kazi katika maisha yetu kwa hatua tatu (Yohana 16:8-11). Kwanza, hutuonyesha dhambi zetu tunazopaswa kuleta kwa Yesu. Pili, hutuonyesha haki ya Kristo, itoshayo kutuokoa. Tatu, humuondoa Shetani na dhambi kutoka katika maisha yetu (Yohana 16:11).
Wazazi wangu walilea watoto wao sita (mimi ni wa tano) kumuamini Mungu na Biblia. Tulijifunza kwamba kulikuwa na mbingu ya kushinda na jehanamu ya kuepuka. Hata hivyo, hatukutafuta uhusiano na Mungu au kumuamini. Kaka wa mama yangu, mjomba wangu, alioa Mwadventista wa Sabato. Siku moja mjomba wangu Harold alimwambia mkewe angemthibitishia kutoka kwenye Biblia kwamba hakupaswa kuitunza Sabato (Jumamosi). Hata hivyo, baada ya kujifuna sana, aligundua kwamba Sabato ya kweli ya Biblia kwa hakika ilikuwa Jumamosi. Baadaye Harold alibatizwa na kuwa Mwandventista wa Sabato.
Baada ya muda mchache Harold alishiriki Imani yake na familia yetu, na kwa kadri nilivyojitahidi, sikuweza kupata njia ya kukanusha mafundisho ya Biblia kuhusu Sabato. Sikutaka kuitunza Sabato. Ilikuwa ni usumbufu katika mipango yangu. Baada ya muda udhihirisho wa Roho Mtakatifu kwamba nilikuwa mdhambi niliyestahili uharibifu ulijikita ndani ya akili na moyo wangu. Nilifahamu kuwa sikuwa nikimfuata Mungu, na nilifahamu kuwa sitaokolewa. Wakati huo barua ilifika kutoka kwa mjomba wangu Harold, na alielezea vile Mbingu itakavyokuwa kupitia Biblia kama mamlaka yake.
Kadri nilivyosikiliza maelezo ya Mbingu, nilihisi shauku kubwa ya kutoa maisha yangu kwa Mungu. Kisha nikasikia sauti ya Mungu ndani ya moyo wangu kwa uwazi kama vile ni mtu alikuwa ameketi kando yangu. “Ni utoe maisha yako kwangu sasa, au hutayatoa kamwe.” Ghafla nilihisi wasiwasi mkuu. Nilikuwa nikiacha Mbingu kwa vitu vya dunia hii. Niliinuka kutoka kwenye kiti changu, nikaelekea chumbani kwangu, na kufunga mlango. Nilipiga magoti kando ya kitanda changu na kuomba kwa mara ya kwanza kutoka moyoni mwangu. Nilipambana kufahamu hasa cha kusema, lakini hatimaye niliomba, “Yesu mpendwa, ninatakuwa kuwa vile unahitaji niwe. Ninataka kutenda vile utakavyo nitende, na ninataka kwenda pale utakapo niende.”
Dakika niliyosema ombi hilo, nilihisi badiliko likipita katika mwili wangu. Hasira na ukorofi wangu wa awali uliachiliwa, na upendo, Amani, na furaha ya Mungu iliujaza moyo wangu. Nilifahamu kwamba Mungu alisikia ombi langu, na nilifahamu nilichopaswa kutenda. Niliinuka magotini na kwenda kumueleza mama yangu habari zile njema – kwamba sasa ningeishi kwa ajili ya Yesu na kuanza kuitunza Sabato. Machozi ya furaha yalitiririka usoni mwake. Ndani ya siku kadhaa nilanza kuachia kila kifungo cha dhambi kilichoniunganisha na dunia. Baadhi ya watu hawakuelewa uamuzi wangu, na njia mbele yangu haikuwa wazi kabisa, bali dhamiri yangu ilikuwa wazi, na furaha iliujaza moyo wangu! Baadae nilijifunza pamoja na Mchungaji wa Kiadventista na kuanza kuelewa Zaidi kuhusu nia ya Mungu kwa maisha yangu. Hatimaye nilibatizwa na kuwa mshiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato. Ni uamuzi bora Zaidi niliowahi kufanya!
Mafungu ya Biblia ya Kuombea Siku moja
Paulo aliuliza watu 12 kutoka Efeso, “Je! Mlipokea Roho Mtakatifu mlipoamini?” (Matendo 19:2). Je, wewe ungejibu vipi? Wale Waefeso walisema, “La, hata kusikia kwamba kuna Roho Mtakatifu hatukusikia.”
Nyimbo Zinazopendekezwa:

- Yohana 16:8-11 – Ni kazi ya Roho Mtakatifu kutuhakikishia dhambi zetu na kutuongoza kwa Yesu.
- Warumi 3:10, 23 – Hakuna mwenye haki, kwani wote tumetenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu.
- Warumi 6:23 – Mshahara wa dhambi ni mauti, bali karama ya Mungu ni uzima wa milele katika Kristo Yesu.
- Yohana 3:16 – Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa mwanawe wa pekee, ili kila amuaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
- Waefeso 2:8, 9 – Tunaokolewa kwa neema kwa njia ya Imani, wala si kwa wema wetu. Ni kipawa cha Mungu, si matendo yetu.
- 1 Yohana 5:11-13 – Ikiwa tumekubali Yesu kwa Imani, tunafahamu kuwa tuna uzima wa milele.
- Warumi 8:16 – Roho mwenyewe hushuhudia, na tunafahamu kuwa sisi ni wana na binti za Mungu.
- Kila siku, kadri tunavyomgeukia Yesu na kuomba, tunapokea msahama na neema. Kama watoto wa Israeli walivyotoka kila siku kupokea mana kutoka mbinguni, vivyo hivyo kila siku tunafanya upya uhusiano wetu na Yesu, Mkate wa Uzima (Yohana 6:58). Kupitia uwepo wa Roho Mtakatifu unaozunguka katika maisha yetu, tunaungama dhambi zetu kwa Mungu, na kukubali haki ya Kristo kwa niaba yetu, na tunaweza kushinda majaribu ya shetani (Wagalatia 5:16). Mapendekezo ya Maombi
- Mpendwa Baba wa mbinguni, ninafahamu kuwa mimi ni mwenye dhambi. Tafadhali nisamehe dhambi zangu zote kama ulivyoahidi kutenda (1 Yohana 1:9). Asante! Pia uliahidi kunipatia uzima wa milele ikiwa nitamkubali Yesu kama Mwokozi wangu. Leo ninamchagua Yesu. Ninasubiri kwa hamu ujio wa Yesu!
- Mpendwa Yesu, ninataka kutembea na wewe daima katika uwepo wa Roho Mtakatifu ili niweze kuhisi ujio wa Shetani na malaika zake waovu. Nipatie nguvu zako ili niweze kutambua na kushinda majaribu (Yakobo 4:7)
- Sasa ninakuamini, Bwana, kwa ajili ya wokovu wangu. Naomba niwe na uhakika wa furaha na kamilifu ili kwamba maisha yangu yaweze kuvuta roho zilizopotea kuja kwako.
- Mpendwa Baba, watu wengi katika makanisa ya ulimwengu huu wana dini tu. Hawamfahamu Yesu na neema yake iokoayo. Tafadhali mtume Roho wako Mtakatifu awadhihirishie dhambi zao na kuwaongoza kwa Yesu. Wafanye waogope sherehe za kawaida. Wawe na njaa ya uwepo halisi wa Mungu katika maisha yao.
- Bwana, tunaomba kwa ajili ya wale walio katika vifungo vya kiroho na kiakili waweze kuwekwa huru kutoka kwenye hatia na vifungo vingine.
- Tafadhali inua wanafuzi Wawaldensia wa siku za sasa, walio tayari kukutumikia katika maeneo magumu.
- Tunaomba kwamba Mungu ainue wamisionari wenye hekima walio tayari kufanya kazi kati ya makundi 746 ya watu katika nchi 20 za Mashariki ya Kati.
- Tunaomba kwa ajili ya Harakati 1,000 za Kimisionari katika Divisheni ya Kaskazini mwa Asia-Pasifiki na Divisheni ya Kusini mwa Asia-Pasifiki. Tunaomba vijana hawa watiwe nguvu kutenda kazi ya Mungu.
- Tunaomba kwa ajili ya watu milioni 202 katika miji 41 ambayo haijafikiwa Zaidi katika Divisheni ya Asia-Pasifiki waweze kumfahamu Yesu.
- Tunaombea vijana wanaoishi kwa hatari kwa ajili ya Bwana kupitia Harakati ya OYiM (One Year in Mission) na harakati ya Mission Caleb.
- Pia tunaomba kwa ajili ya orodha zetu za watu saba au Zaidi [taja majina kama inawezekana]
- Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa:
- Kuwa na Yesu Mwokozi #51,
- Roho Mtakatifu #41
- Taamini Nitii Pia #128
No comments
Post a Comment