UZINDUZI WA DVD YA UFUNUO CHOIR WAFANA, MGENI RASMI ASHINDWA KUJIZUIA...
Kwaya ya Ufunuo kutoka katika kanisa la Waadventista Wasabato - Mtwara mjini, leo imefanya uzinduzi wa DVD toleo la 1 iitwayo Kando Ya Bahari.
Katika uzinduzi huo mgeni rasmi alikuwa mkurugenzi wa manispaa ya Mtwara Mikindani Mh. Limbakisye Shimwela ambaye alionesha kuvutiwa sana na waimbaji hao. Kabla ya kutoa hutuba yake mkurugenzi aliomba kwaya irudie wimbo uitwao "Nani atakaye simama". Bwana Shimwela alisema kuwa wimbo huo umembariki sana na atakuwa akiusikiliza mara kwa mara nyumbani kwake.
Aidha Bwana Shimwela amewaasa washiriki kuomba sana ili taifa liwe salama hasa katika kipindi hiki ambacho kuna masuala mengi na makubwa ya kitaifa kama vile uandikishwaji wa daftari la kudumu, upigaji kura ya katiba ya nchi na uchaguzi mkuu. Mkurugenzi pia amewaalika washiriki kushiriki katika masuala mbalimbali ya kitaifa.
Akizungumzia uzoefu wake katika uimbaji Bwana Shimwela amesema amewahi kuwa mwimbaji na anajua changamoto zilizopo katika uimbaji ila amewataka waimbaji wajitoe katika kuifanya kazi ya Mungu ulimwenguni pote.
Mara baada ya uzinduzi Mheshimiwa Shimwela alishindwa kujizuia na kujikuta akiungana na kwaya katika marching iliyoleta mvuto wa pekee na kufanya uzinduzi uwe na mvuto wa aina yake.
Katika uzinduzi huu jumla ya shilingi 7,038,000/= (Milioni saba na elfu thelathini na nane) zimepatikana ikiwa ni jumla ya ahadi na fedha taslimu.
Tafadhali usiikose DVD hii yapekee.

No comments
Post a Comment