PICHA ZA MATUKIO MBALIMBALI KTK SABATO YA 05/10/2019
Karibu katika blog ya kanisa la Waadventista Wasabato Mtwara. KAMA BADO HUJAPAKUA APP YA MTWARA SDA KATIKA SIMU YAKO PAKUA SASA KWA KU BOFYA HAPA
Leo tarehe 05/10/2019 imekuwa ni Sabato ya pekee sana baada ya kutembelewa na kwaya kuu ya Kanisa la Kiinjili la Kirutheri Tanzania (KKKT) - Mtwara walioshirikiana nasi katika ibada ya leo tangu asubuhi mpaka katika vipindi vya mchana.
Kwaya nyingine zilizohudumu ni kwaya ya Kanisa la Mtwara (Ufunuo Choir) pamoja na kikundi cha The Hope Generation toka Mtwara SDA. Aidha tulibarikiwa kwa vipindi mbalimbali ambapo darasa la waalimu katika Shule ya Sabato liliongozwa na Mwalimu Yohana Raphael Magambo, Kipindi cha uimbaji (Nyimbo za Kristo) kiliongozwa na Mwalimu Joseph Kazimili, Shule ya Sabato Mezani iliongozwa na kwaya ya Ufunuo na tulikuwa na darasa moja la lesson lililo ongozwa na Mwalimu Yohana Raphael Magambo
Neno la Mungu katika ibada kuu lililetwa na Mchungaji Gipson kisha kilifuatia kipindi cha mapumziko kwaajili ya chakula cha mchana na mara baada ya mapumziko kipindi cha uimbaji kilichosimamiwa na Mwalimu Eliya Charles kilifuatia ambapo kwaya zote zilipata nafasi ya kuimba kisha kipindi cha maombi kilifuatia kikiongozwana na Pr Gipson na Mwinjilisti Michael (Ikumbukwe kuwa leo ni Sabato maalumu ya maombi ulimwenguni)
Angalia picha za matukio mbalimbali hapa chini kisha share.