Usikose Ibada ya kufungua Sabato

Habari, Hongera kwa kufanya kazi kwa muda wa siku sita, Nachukua fursa hii kukukaribisha katika ibada ya ufunguzi wa Sabato ifikapo saa 11:30 jioni. Mara baada ya Ibada ya ufunguzi, tutaendelea na mkutano wa injili kwa njia ya Sattelite unaorushwa kutoka jijini Mbeya. Kituo cha Mkutano ni Mtwara SDA.
MATANGAZO MENGINE MUHIMU
  • Waimbaji wote wa kwaya za kanisa mnatakiwa kufika kanisani saa tisa alasiri kwa ajili ya maandalizi ya chakula cha wageni yaani KKKT Choir. Tunategemea kupata ushirikiano wa dhati kutoka kwenu.maelekezo yote yako kwa dada Mwanahamisi Shaibu.
  • Pia Mashemasi wa,zamu mnaombwa kufika kwa ajili ya maandalizi ya sabato. Changamoto kubwa kwa sasa ni Maji.hivyo mnaombwa kufika kwa wakati ili tushirikiane kukabiliana na changamoto hizo.
Barikiweni kwa utekelezaji.
Kwa niaba ya uongozi
Fadhili Taramo

Powered by Blogger.