Matangazo ya kanisa: Sabato ya tarehe 11/01/2020


Ukaribisho:

Wageni kwa Wenyeji karibuni nyote katika Ibada   Takatifu ya Sabato ya leo.

Bwana yuko ndani ya hekalu lake Takatifu,DUNIA YOTE NA INYAMAZE KIMYA MBELE ZAKE. HABAKUKI 2:20

1. IDARA YA WATOTO BADO INAUHITAJI WA VITI VYA WATOTO, HIVYO WASHIRIKI TUNAOMBA MUENDELEE KUJITOA KWA AJILI YA UNUNUZI WA VITI.
2. IDARA YA VIJANA (SEC) INATANGAZA KUANZA KWA USAJILI WA WANACHAMA NA KOZI KWA MWAKA 2020, HIVYO WATAKAO SAJILIWA WOTE WAANZE KUJAZA FOMU KUTOKA KWA VIONGOZI WAO.
3. KUTAKUWA NA WEEKEND CAMP KWA IDARA YA VIJANA (SEC) KWA MWAKA 2020. KIINGILIO NI TSHS 5,000/= PESA YA CHAKULA NI TSHS 10,000/=. TAARIFA ZAIDI TUTAZIPATA KUTOKA KWA VIONGOZI WA IDARA.
4. KUTAKUWA NA KONGAMANO LA UIMBAJI              LITAKOFANYIKIA LIWALE MWEZI WA NNE KATIKA KIPINDI CHA PASAKA WAIMBAJI WOTE WAJIANDAE, KIIGILIO NI TSHS 150,000/= KWA KWAYA MOJA.
5. FOMU ZA KUJIUNGA NA KWAYA ZA KANISA  ZINAPATIKANA KWA KATIBU WA KANISA WOTE WANAOWIWA KUMUIMBIA MUNGU 2020 WAJAZE  NA KURUDISHA KWA KATIBU. WAIMBAJI WANAOENDELEA PIA WANASHAURIWA KUJAZA FOMU.
6. WANA WA KIKE WOTE WABAKI MARA BAADA YA IBADA.

WAGONJWA:
TUENDELEE KUWAOMBEA WAGONJWA WOTE NA KUWATEMBELEA KWA AJILI YA FARAJA.

Vikao/Semina/Mikutano


1. JUMA LA MAOMBI NA KUFUNGA LILILOANZA TAREHE 08/01/2010 linaendelea MPAKA SABATO YA TAREHE 18.01.2020. washiriki na waumini tuhudhurie KATIKA MASOMO YA JUMA HILI SAA 11 JIONI KILA SIKU.
2. KUTAKUWA NA BARAZA LA BAJETI TAREHE 19/01/2020. WAKUU WA IDARA WAANDAE BAJETI NA KUWASILISHA KWA WAZEE WA IDARA HUSIKA.

3. Kutakuwa na kikao cha mashemasi jumapili ya tarehe 12/01/2020 saa nne asubuhi.

TANGAZO LA NDOA
TUNATANGAZA KUSUDIO LA KUFUNGA NDOA TAKATIFU KWA MARA YA nne KATI YA NDUGU JAMES PETER LAINA AMBAYE NI MSHIRIKI WETU NA SUZAN SALUM; ITAKAYOFUNGWA JUMAPILI YA TAREHE 12.01.2020 KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO MTWARA.

MZEE WA ZAMU:   DANIEL JOSHUA

No comments

Powered by Blogger.