Siku 10 za maombi: Siku ya Tatu - Ijumaa - (10/01/2020)
Ushindi Kupitia kwa Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Basi nasema, Enendeni kwa Roho, wala hamtazitimiza kamwe tamaa za mwili.” Wagalatia 5:16.
Ushuhuda
“Hakuna kitu ndani yake [Yesu] kilichoitikia madanganyo ya Shetani. Hakuridhia dhambi. Hakujitoa kwa dhambi hata kwa wazo tu. Hivyo inaweza kuwa kwetu. Ubinadamu wa Kristo uliunganishwa na uungu; Roho Mtakatifu aliyeishi ndani yake alimuandaa kwa ajili ya pambano. Na alikuja kutufanya kuwa washiriki wa asili ya uungu. Tutakapoungana naye kwa Imani, dhambi haitakuwa na nguvu dhidi yetu. Mungu huushikilia mkono wa Imani ndaniyetu ili auongoze kushikilia kwa haraka utakatifu wa Kristo, ili tuweze kupata ukamilifu wa tabia” (Ellen White, The Desire of Ages, uk. 123).
Jerry alikuwa mfanyakazi mwenye bidii. Alitumia muda mwingi wa utu uzima wake kama mfanyakazi wa vifaa vya chuma akijenga madaraja na magorofa. Alikuwa ni mtu aliyepanda mamia ya futi juu ya nchi kwenye chuma nyembamba na kuichomelea kwenye chuma nyingine. Ingawa Jerry alikuwa na kipaji sana na mtenda kazi mashuhuri, aliharibu mwili wake kwa pombe, tumbaku, madawa, wanawake, na maisha yasiyofaa. Wakati wo wote Mkristo alipokuja kazini, Jerry alimtesa kwa maneno na kihisia, akitegemea kumfanya aiache kazi hiyo. Jerry alichukia Ukristo na Wakristo.
Kadri Jerry alivyokaribia miaka 50, alianza kupata msongo. Siku moja aliamua kusitisha maisha yake. Kadri alivyokuwa akiendesha kuelekea nyumbani ili kujiua, aliona kibao cha Kanisa la Waadventista wa Sabato barbarani. Roho Mtakatifu aliweka wazo akilini mwake: “Pengine wanaweza kunisaidia.” Hivyo Jerry aliegesha gari sehemu sahihi mara tu shule ya kansia ilipokuwa ikimaliza ratiba zake kwa siku hiyo, alimkaribia mkuu wa shule, na kunong’oneza kitu kuhusiana na kuhitaji msaada.
Mkuu alimpatia Jerry namba yangu ya simu na kumwambia, “Hii ni namba ya mchungaji wetu. Tafadhali mpigie.” Jerry alipopiga usiku ule, alinieleza kwamba aikuwa kwenye matatizo na akauliza kama naweza kumsaidia. Nilimpigia mzee wa kanisa, na pamoja tulienda nyumbani kwa Jerry.
Jerry alitueleza kila kitu na kuongeza, “Siamini kwamba nimeanguka sana kiasi cha kuwa na mchungaji nyumbani kwangu.” Alisema alijaribu kila kitu dunia iliweza kutoa bila kupata suluhisho, hivyo aliamua kusitisha maisha yake. Nikasema, “Jerry haujajaribu kila kitu kwa sababu haujamjaribu Yesu.” “Upo sahihi,” alihamaki, “Sijamjaribu Yesu. Hivyo, ninapaswa kufanya nini kumjaribu Yesu?” nilishiriki ujumbe rahisi wa injili na kumuliza, “Je, kuna sababu yo yote ya kukufanya usitake kumpokea Yesu katika maisha yako?” Jerry alisema, “Hapana, kwa sababu asipotenda kitu kwa ajili yangu usiku wa le, nitasitisha maisha yangu.”
Huku nikimualika Jerry kupiga magoti pamoja nasi, nilimuomba arudie ombi baada yangu. Baada tu ya sisi kusema “Amina,” Jerry alishika mkono wangu na kusema, “Umeona?” “Nimeona nini?” niliuliza. “Niliposema tu ‘Amina,’ nilifungua macho yangu na kuona mtu akipita juu ya kichwa changu akiwa na uso wa ukali, na kasha akapotelea kwenye dari. Unapaswa kuniamini!” “Ninakuamini, Jerry,” nilisema. “Unajisikiaje sasa?”Baada ya muda wa kutafakari alisema, “Ninajisikia vizuri, vizuri sana. Sijajisikia vizuri hivi kwa muda mrefu sana, kama nilishawahi. Nini kimenitokea?” Nilimueleza, “Jerry, umemuomba Yesu aingie katika maisha yako na kukusamehe dhambi zako. Sasa anaishi ndani yako. Roho ya uovu uliyoiona ilikuwa ikijaribu kukufanya usitishe maisha yako, lakini Yesu ameiondoa.”
Furaha kuu ilijaa nyumbani kwa Jerry usiku ule, furaha nyingi kiasi cha Jerry kushindwa kulala. Alizunguka nyumbani kwake akiondoa pombe, madawa, magazeti, na vitu vingine vyote ambavyo aliona ni vyenye dhambi. Aliweka vitu vyote katika mfuko wa plastiki na kuvizika futi sita kwenda chini katika shamba lake. Siku iliyofuata aliendesha gari kuelekea kwenye duka la mimea na kununua mti ili kuupanda sehemu alipozika vitu vyote vile. Nilipomtembelea tena alinionyesha mti ule na kusema, “Mchungaji, shimo hilo na mti huo unawakilisha maisha yangu. Jerry wa zamani amezikwa hapo chini na mti huo mpya wa matunda unawakilisha Jerry mpya kwa sababu sasa ninaishi maisha mapya.”
Mafungu ya Biblia ya Kuombea
Mapendekezo ya Maombi
Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa
Yesu Unipendaye #30,
Yesu Nataka Kutakaswa Sana #114
Twae Wangu Uzima #146

- Yohana 16:8-11 – Ni kazi ya Roho Mtakatifu kutuhakikisha kwa dhambi zetu na kutuongoza kwa Yesu.
- Ezekieli 36:25, 26 – Tumeahidiwa moyo mpya, akili mpya, na maisha mapya.
- 2 Wakorintho 5:17 – Mtu ye yote akiwa ndani ya Kristo, amekuwa kiumbe kipya. Ya kale yamepita.
- Yohana 8:36 – Unaweza kuwa huru kwelikweli kupitia kwa Yesu Kristo.
- 1 Wathesalonike 4:3 – Ni nia ya Mungu kwamba wewe uingie katika ushindi dhidi ya dhambi.
- Warumi 6:14 – Dhambi haitakutawala tena.
- Mathayo 5:29, 30 – Jitenge kutoka kwa mtu au kitu cho chote kinachokushawishi kuingia dhambini.
- Warumi 12:21 – Weka watu na vitu chanya badala ya watu na vitu hasi
- Wagalatia 5:19-26 – Tamaa za mwili zilizo za uovu zinaweza kufunikwa kwa tunda la Roho.
- Kila siku, kadri tunavyomgeukia Yesu na kuomba, tunapokea msahama na neema. Kama watoto wa Israeli walivyotoka kila siku kupokea mana kutoka mbinguni, vivyo hivyo kila siku tunafanya upya uhusiano wetu na Yesu, Mkate wa Uzima (Yohana 6:58). Kupitia uwepo wa Roho Mtakatifu unaozunguka katika maisha yetu, tunaungama dhambi zetu kwa Mungu, na kukubali haki ya Kristo kwa niaba yetu, na tunaweza kushinda majaribu ya shetani (Wagalatia 5:16).
Mapendekezo ya Maombi
- Mpendwa Bwana, ninafahamu kwamba ni mapenzi yako mimi kushinda dhambi kwa nguvu zako. Tafadhali nijaze kwa Roho wako Mtakatifu na niongoze katika kweli yote (Yohana 16:13).
- Katika jina la Yesu na kupitia kwa damu yake, ninamkemea Shetani na roho zake za uovu katika maisha yangu. Tafadhali, Bwana, muondoe muovu ndani ya maisha yangu na nyumba yangu. Ruhusu kweli na haki pekee zikae ndani yangu.
- Mpendwa Bwana, jaza maisha yangu kwa uwepo wa Roho Mtakatifu. Naomba nguvu zake zitiririke kupitia kwangu na kuhudumu kwa wale ambao bado wamefungwa katika dhambi. Walete kwa Yesu ili vifungo vyao viweze kuvunjwa.
- Bwana, tusaidie kuwa na uvumilivu na upendo, tukionyesha upendo na huruma yako kwa wale wanaotukasirisha au kutushutumu.
- Tunaomba kwa ajili ya wale wanaohudumia wazee wao wanafamilia wagonjwa. Wapatie uvumilivu, nguvu, na upendo.
- Bwana, tafadhali punguza wasiwasi wa wale wanaopitia magonjwa yasiyotibika. Wapatie ujasiri na Amani ya Yesu.
- Tunaomba kwa ajili ya Idara ya Shule ya Sabato na Idara ya Huduma binafsi ya kila kanisa mahalia kadri wanavyotafuta mpango wa Mungu na kuzifikia jamii zao kwa huduma za upendo, Kujifunza Biblia, na ushuhudiaji binafsi.
- Tunaomba kwa ajili ya ubatizo wa Roho Mtakatifu kwa vijana wetu na viongozi vijana kama ilivyoahidiwa katika Matendo 1:8. Na tunaomba hasa kwa ajili ya mibaraka ya Mungu kwa vijana waliohusika katika shughuli ya “Give Him 20” (Mpatie 20) na mipango mingine ya maombi.
- Bwana, tafadhali tuonyeshe mkakati uliokubaliwa na Mungu wa kufikia Yeriko a dunia kwa Ujumbe wa Malaika Watatu na kuongoza akina Rahabu katika kila mji kwenye wokovu katika Kristo.
- Tafadhali bariki siku 100 za Maombi (Machi 27 – Julai 4) kuelekea kwenye Mkutano wa Uchaguzi wa Konferensi Kuu. Mwaga Roho Wako Mtakatifu kadri tunavyoomba hekima na ujio wako ulio karibu.
- Pia tunaomba wka ajili ya orodha yetu ya watu saba au Zaidi [taja majina kama inawezekana]
Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa
Yesu Unipendaye #30,
Yesu Nataka Kutakaswa Sana #114
Twae Wangu Uzima #146
No comments
Post a Comment