Siku 10 za maombi: Siku ya Nne - Jumamosi - (11/01/2020)
Ubatizo wa Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Hata alipokuwa amekutana nao aliwaagiza wasitoke Yerusalemu, bali waingoje ahadi ya Baba, ambayo mlisikia habari zake kwangu; ya kwamba Yohana alibatiza kwa maji, bali ninyi mtabatizwa katika Roho Mtakatifu baada ya siku hizi chache.” Matendo 1:4, 5.
Ushuhuda
“Unapokuwa umepokea ubatizo wa Roho Mtakatifu, utaelewa zaidi furaha za wokovu kuliko ulivyokuwa ukifahamu maisha yako yote” (Ellen White, Manuscript Releases, vol 5, uk. 231).
Nilimtembelea mtu aliyekuwa akikaribia kufariki kwa ugonjwa usiotibika. Niliomba na kujaribu kumtia moyo kwa upendo na rehema za Mungu, lakini nilipoondoka nyumbani kwake, nilikumbwa na namna nilivyokuwa nikihisi kutokuwa na nguvu katika hali ile – na namna Wakristo wengi wanaonekana kutokuwa na nguvu. Kadri nilivyolinganisha maisha yangu na maisha ya Wakristo wngine pamoja na maisha ya Wakristo wa Agano Jipya, tofauti ilikuwa ikishangaza. Kama matokeo ya ugeni ule, niliamua kujifunza kwa kina somo la Roho Mtakatifu katika Biblia. Hatimaye nilijifunza mafungu 273 katika lugha za asili ambayo huzungumza moja kwa moja katika kazi ya Roho Mtakatifu, na niligundua zaidi ya nukuu za pekee 2,000 za maandiko ya Ellen White juu ya mada hii.
Katika kujifunza kwangu Biblia niligundua ubatizo wa Roho Mtakatifu. Uzoefu ule ulibalisha maisha ya Petro, Paulo, na kila mmoja aliyepokea Roho wa Mungu kwa ukamilifu. Hata Yesu alijazwa na Roho Mtakatifu, kwani kabla ya Roho Mtakatifu kushuka kwake kwa mfano wa hua, alidumu kuwa katika karakana ya seremala. Baada ya Roho kushuka juu yake, Yesu alitenda kazi ya Masihi.
Katika visa vya Biblia, daima tunapata uthibitisho unaoonyesha kwamba nguvu ya Roho Mtakatifu imetolewa. Usiku wa siku ya Ijumaa majira ya saa 4, binti yetu mwenye umri wa miaka 8 alimuita Mama yake. Mke wangu alipokuwa akimuendea, niliamua kwenda ofisini kwangu na kuomba. Nilipokuwa nikiomba, nilihisi uwepo mtakatifu wa Yesu ukiingia kwenye chumba kile. Nilianza kunena na Bwana kwa hamasa kuu na njaa ya uwepo wa Roho wake katika maisha yangu. Ghafla nilimuona Yesu katika mlango wa kanisa langu kwa upendo akiweka mkono wake wenye alama za misumari kwenye mabega ya kila mshiriki akiwa na mtazamo wa neema na ukaribisho. Yesu aliniuliza, “Je, unawapenda watu wangu?” ningeweza kusema niliwapenda, lakini ilinibidi kukubali kwamba baadhi yao ilikuwa vigumu kuwapenda.
Machozi yalianza kunitiririka kadri nilivyoungama dhambi yangu. Kisha niliona miguu iliyokuwa na alama za misumari ikisimama kwenye mimbara ambayo nilihubiri kila juma. Yesu alisema, “Nilikufa ili nisamehe na kuokoa watu wa dunia hii. Je, unahubiri injili kila siku kwa shauku kwa ajili ya nafsi zilizopotea?” ningeweza kusema ilikuwa shauku yangu kuhubiri injili kwa uharaka wa kuokoa waliopotea, lakini nilijihisi kutostahili katika uwepo wake. Machozi yalitirirka kadri nilivyoungama dhambi zangu kwa Yesu. Kasha niliona taji ya miba ikilazimishwa katika kichwa chake. Nilimsikia Yesu akisema, “Nilijinyenyekeza hata mauti ya msalaba. Je, unatafuta sifa kutoka kwa wanadamu?” ningeweza kusema sikutaka sifa za wanadamu, lakini kwa machozi nilikubali kuwa nilipambana na kiburi. Nilijihisi kutostahili na kutokukubalika katika uwepo wake, na mahozi yalinitiririka ziadi. Ghafla Yesu alivua kando vazi lake, na nikaona upande ambapo mkuki ulimchoma. Alisema, “Wale wanaonijia sitawatupa kamwe.”
Kisha nilihisi upendo kamili na ukubali wa Bwana kuliko nilivyowahi kuhisi hapo kabla. Nilifahamu kuwa dhambi zangu zilisamehewa, na nilifahamu kuwa alinikubali. Nilizama katika ufunuo huo wakati nilipomsikia mke wangu akishuka ngazi. Nilitazama saa; ilikuwa ni saa 6 usiku. Masaa mawili yalionekana kama dakika chache tu. Sikuwa tayari kuzungumza kuhusu kilichotokea, hivyo nilirudi kitandani na kugeuza mgongo wangu mlangoni ili mke wangu asione kama nilikuwa macho. Alipoingia chumbani, aliuliza, “Nini kimekutokea?” Nilisema, “Unamaanisha nini?” Alisema, “Ninafahamu kuna kitu kimekutokea. Ninaona. Nini kimetokea?” Hivyo nilimweleza kila kitu, na wakati huo huo mke wangu alitoka kuelekea sebuleni na kuomba mwenyewe. Niliweza kumsikia akimuita Mungu aweze kubarikiwa pia.
Siku iliyofuata, Sabato, nilihisi nguvu ya Mungu kadri nilipohubiri somo langu. Baadhi ya watu walifanya maamuzi kwa ajili ya Kristo siku ile. Baadaye mtu mmoja aliuliza, “Mchungaji, kuna kitu kilikutokea jana usiku?” Nikiwa nimeshangaa, nilisema, “Kwa nini unauliza?” Alisema, “Ninafahamu kuna kitu kitakuwa kimekutoka jana usiku. Wakati wote ulipokuwa ukihubiri, niliona mng’ao katika uso wako.” Niliposhiriki kilichotokea, alisema, “Kwa hakika Bwana amekutembelea.” Mwaka ule watu 37 walitoa maisha yao kwa Yesu. Katika miaka iliyofuata baada ya usiku ule, mamia ya watu wamefanya maamuzi kwa ajili ya Kristo. Bwana Yesu asifiwe milele!
Mafungu ya Biblia ya Kuombea.
Nyimbo Zinazopendekezwa
Tubatize Upya #189,
Ati Kuna Mvua Njema #39
Roho Yangu Amka Sasa #66

- Luka 3:21, 22 - Baada ya ubatizo wake, Yesu aliomba Roho Mtakatifu aje juu yake.
- Matendo 1:5-8 – Utapokea nguvu akisha kukujilia Roho Mtakatifu. x Matendo 2:1-4 – Na wote wakajazwa Roho Mtakatifu na kuanza kunena kwa lugha mbalimbali.
- Matendo 4:31 – Kanisa la awali lilipokea nguvu kadri lilivyoomba kwa ajili ya Roho wa Mungu kuja juu yao.
- Matendo 8:15-17 – Walibatizwa kwa maji katika jina la Yesu, bali walihitaji Roho Mtakatifu.
- Luka 11:11-13 – Ubatizo wa Roho Mtakatifu unatolewa kwa wale wanaomtafuta kupitia maombi.
- Matendo 5:31, 32 – Roho Mtakatifu atatolewa kwa wale walio tayari kutii. Mapendekezo ya Maombi
- Mpendwa Baba, tafadhali nibatize katika Roho Mtakatifu ili niweze kuishi na kukupenda kwa mafanikio.
- Ni shauku yangu kuu, Bwana Yesu, kwamba nikuwakilishe vyema kwa ulimwengu. Tafadhali andaa moyo wangu kumpokea Roho Mtakatifu na kushiriki upendo wako na watu wengine katika maisha yangu.
- Tafadhali niongoze katika kweli yote ili daima niweze kutenda yale yapendezayo machoni pako. Mruhusu Roho wako Mtakatifu adhihirishe kwangu kile unachotaka nifahamu na unachotaka nishiriki na wengine. Naomba misimamo na mizigo yangu itoke moyoni mwako na si kutoka kwenye matendo yangu ya ubinafsi.
- Tunamba kwamba wapendwa wetu walioiacha Imani wakumbuke inavyokuwa wakiwa katika ushirika na wewe na kutamani kuunganika tena na wewe. Wasaidie kuhisi na kukubali upendo na msamaha wako.
- Bwana, tunaomba ulinzi wako kwa wamisionari wanaofanya kazi katika maeneo hatarishi.
- Tunaomba kwa ajili ya watu milioni 16 katika miji 6 ambayo haijafikiwa Zaidi ya Divisheni ya Kusini mwa Pasifiki. Tunaomba kwa ajili ya ubatizo wa kila siku wa Roho Mtakatifu kwa washiriki kadri wanavyowafikia kwa upendo wale ambao hawajafikiwa bado.
- Tunaomba kwamba Roho Mtakatifu atusaidia kufahamu namna ya kuwafikia watu milioni 406 katika miji 105 isiyofikiwa Zaidi ya Divisheni ya Kaskazini mwa Asia-Pasifiki.
- Tafadhali bariki Huduma za Chaplensia za Kiadventista kadri zinavyosimamia chaplensia na washiriki wenye shauku katika kuhudumia wale walio katika magereza.
- Pia tunaomba kwa ajili ya orodha yetu ya watu saba au Zaidi [taja majina kama inawezekana]
- Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa
Tubatize Upya #189,
Ati Kuna Mvua Njema #39
Roho Yangu Amka Sasa #66
No comments
Post a Comment