Siku 10 za maombi: Siku ya Nane - Jumatano - (15/01/2020)
Kujisalimisha kwa Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Kwa sababu hiyo nawaambia, Kila dhambi na kila neno la kufuru watasamehewa wanadamu, ila kwa kumkufuru Roho hawatasamehewa.” Mathayo 12:32.
Ushuhuda
“Hakuna mtu anapaswa kuitazama dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu kama kitu cha ajabo na kisichoelezeka. Dhambi dhidi ya Roho Mtakatifu ni dhambi ya kudumu kukata kuitikia wito wa kutubu” (Ellen White, SDA Bible Commentary, vol 5, uk. 1093).
Kila mtu aliyejazwa roho hutenda makosa nyakati zingine. Ibrahimu, Musa, Daudi, na Petro wote walikuwa na matatizo katika tabia na kushindwa mara kwa mara katika saa ya majaribu. Hata Yesu alijaribiwa (Mathayo 4), japo hakukubali kujaribiwa. Hivyo, kwa sababu tu tunatembea katika Roho kwa wakati huu haimaanishi kwamba tumevuka nafasi ya kuweza kutenda makosa, na kosa si sawa na kufanya mioyo yetu kuwa migumu katika dhambi.
Mwanamke mmoja katika miaka yake ya mwisho alikuwa mtu asiyejali, aliyekata tamaa, na mwenye hasira. Alikuwa na uvumilivu kidogo kwa wengiine isipokuwa marafiki zake wa karibu kwa miaka hiyo. Wageni walipokuja kanisani, mara nyingi alitoa maneno ya kashfa kuhusiana na watoto wao, mavazi yao, au kitu kingine. Washiriki wapya waliokuwa wamebatizwa na watu wengine walikasirishwa kwa maneno yake ya kashfa na kukosoa. Baadhi walikatishwa tamaa kiasi cha kuwafanya kutokuhudhuria tena kanisani. Wakati wote sikuwa nikifahamu jambo hili hadi kwenye kikao kimoja cha wazee. Niliwauliza wazee kama walifahamu kwa nini watu hawakuwa wakirudi kanisani. Baadhi walinyamaza. Hatimaye mzee mmoja alizungumza: “Mchungaji, tuna mwanamke katika kusanyiko letu asiyeweza kutawala mdomo wake.
Husengenya na kukosoa karibu kila mtu. Hii ndiyo sababu watu hawatarudi katika kanisa letu.” “Jambo hili limeendelea kwa muda gani?” niliuliza. “Kwa miaka mingi,” lilikuwa ndilo jibu. “Ni kwa nini hakuna aliyefanya lo lote kuhusu jambohili?” niliendelea. “Baadhi ya wachungaji wamejaribu, lakini hakujawahi kuwa na badiliko.” “Jambo hili haliwezi kuendelea,” nilisema, “hivyo, hili ndilo ninalopendekeza. Nitakwenda kumtembelea mwanamke huyu na kumuomba abadilishe tabia yake ndani ya majuma mawili. Akiwa tayari kubadilika, jina lake litaletwa katika baraza lijalo kwa ajili ya kunidhamishwa. Je, nyinyi wazee mtaniunga mkono katika hili?” Wazee walikubali kuunga mkono mpango huu.
Nilifanya mipango ya kumtembelea mwanamke huyu kwa ajili ya kumhoji. “Ninafahamu ni kwa nini upo hapa,” alisema mara tu nilipoketi sebuleni kwake. “Unafahamu?” nilijibu. “Ndiyo,” aliendelea kusema, “umekuja hapa kuzungumza kuhusu sababu ya ninavyozungumza na watu.” “Hilo ni sahihi kabisa,” nilisema, “lakini ni kwa namna gani umefahamu hilo?” “Kwa sababu wachungaji wengine wawili wamekuja nyumbani kwangu kuzungumzia suala hilo hilo.” “Kulikuwa na badiliko?” niliuliza. “Hapana, hakuna.” “Kwa nini?” niliuliza. “Kwa sababu nina haki ya kuzungumza ninachoona ni chema, na watu ni wepesi kuhisi tofauti. wanavaa hisia ao katika nguo zao.”
Nilijadili kuhusu tabia ya Mkristo kutumia mafungu kama Waefeso 4:29-31, lakini mwanamke yule bado hakuwa tayari kubadilika. Huku nikiomba moyoni mwangu, nilisema, “Una majuma mawili ya kubadilisha tabia yako, au nitalazimika kupeleka jina lako katika baraza la kanisa kwa ajili ya kunidhamishwa, na nina utegmezi wa wazee wote katika hili.” “Hutafanya hivyo!” alihamaki. “Oh, ndiyo, nitafanya hivyo usipoamua kubadili namna unavyozungumza na watu.” “Siamini kama wazee watakuunga mkono katika hili,” alisema. “Wamekwisha fanya hivyo, na unaweza kuwauliza kama utapenda, lakini hivi ndivyo ilivyo,” nilisema. Udhihirisho huu ulimfanya mwanamke yule atulie na kuwaza kwa ukimya. Kwa upole nilisema, “Sote tunakupenda na tunataka uwe sehemu ya kusanyiko letu, lakini tabia hii inahitaji kubadilika.”
Sabato iliyofuata hakuhudhuria kanisani. Marafiki zake walinikwepa. Nilifahamu kwamba walikuwa wakipambana na hali ile. Sabato iliyofua, kabla tu ya majuma yake mawili kuisha, alikuja kanisani. Nilitembea na kwenda kumsalimu. Uso wake ulikuwa na huzuni, lakini alinishika mkono kwa nguvu. “Mchungaji,” alisema, “Nimefikiria sana ulichosema. Ninataka ufahamu kwamba sasa ninaona kwa uwzi kwamba nimekuwa nikikosea kwa miaka yote hii. Ninatumaini utanisamehe, na nimepanga kuomba msamaha kwa wazee na kanisa zima. Kwa msaada wa Mungu, nitakuwa mwanamke tofauti.” Macho yake yalijawa machozi kwa ukubali huu, na ninafuraha kusema kwamba alikuwa mwaminifu katika ahadi yake. Watu walianza kurejea kanisani, na kusanyiko lilikua kwa haraka.
Mafungu ya Biblia ya Kuombea
Mapendekezo ya Maombi

- Mathayo 12:31, 32 – Kukufuru ni kupuuzia dhambi na kuchukua nafasi ya Mungu (Marko 2:7-11; Yohana 10:33).
- Waebrania 6:4-6 – Watu waliobadilishwa kweli wana uwezo wa kugeuka kutoka kwa Yesu.
- Waebrania 4:7 – Muda sahihi wa kutii sauti ya Roho Mtakatifu ni mara ya kwanza yeye kunena nawe.
- Matendo 7:51 – Usikatae uongozi na maonyo ya Roho Mtakatifu.
- Luka 13:34 – Mpatie Yesu maisha yako kabla haujachelewa, kama ilivyokuwa kwa Yerusalemu
Mapendekezo ya Maombi
- Mpendwa Baba, naomba niisikilize sauti yako daima. Nisamehe pale nilipokuwa msumbufu. Fungua macho na masikio yangu ili nisikilize nia yako na nipatie ujasiri wa kutii.
- Mpendwa Yesu, nisamehe kwa maumivu niliyokusababishia pale ambapo sikuwa tayari kuachia dhambi zangu. Tafadhali usimuondoe Roho wako Mtakatifu kutoka kwangu na naomba ulainishe moyo wangu ili nipokee maelekezo yako.
- Tafadhali samehe kanisa letu pale ambapo hatukuisikiliza sauti yako katika Biblia. Tusaidie sisi kama kusanyiko kujisafisha dhambi na rejesha uwepo wa Roho wako kati yetu.
- Fanya ndani yetu moyo safi, Ee Mungu, na uifanye upya roho sahihi ndani yetu. Usituondoe mbali na uwepo wako na usituondolee Roho wako Mtakatifu. Jeresha kwetu furaha ya wokovu wako. Kisha tutawafundisha waovu njia zako, na watabadilishwa na kurejea kwako (Zaburi 51).
- Baba, tunaingilia kati kwa ajili ya wale wanaoweza kuwa wahanga wa hali fulani au huongozwa na mazoea mabaya. Tafadhali vunja vifungo vinavyowafunga! Tunaomba tuweze kuwarudisha kwako kupitia upendo na kujali kwetu.
- Tafadhali tufundishe namna ya kutangaza misingi yetu ya Imani kwa usawa, ubunifu, na uthibitisho wa kibliblia. Upendo wa Kristo na uwe kiini cha kila kitu tunachokiamini.
- Tunakuomba uandae vijana wa kuanzisha makanisa kwa ajili ya makundi 789 ya watu katika nchi 9 za Divisheni ya Kaskazini wa Amerika.
- Tunakuomba uinue wamisionari wa kitabibu ili kuanzisha makanisa kati ya makundi 830 ya watu katika nchi 11 za Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati.
- Tunakuomba uinue mashujaa wa maombi ili kuomba kwa kuingilia kati kwa ajili ya makundi 2,568 ya watu katika nchi 4 za Divisheni ya Kusini mwa Asia.
- Tunakuomba uinue viongozi wapya walio vijana na bariki semina za Uongozi wa Vijana Wakubwa (Senior Youth Leadership).
- Asante, Baba, kwa kumtuma Roho Mtakatifu kuwabadilisha watu saba katika orodha zetu za maombi.
- Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
No comments
Post a Comment