Siku 10 za maombi: Siku ya Tano - Jumapili - (12/01/2020)
Tunda la Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria.” Wagalatia 5:22, 23.
Ushuhuda
“Kweli inapopendwa na kuthaminiwa, na kuchukuliwa kama mali takatifu, ni wazi kwamba Roho Mtakatifu ndiye ameipanda ndani ya moyo. Kisha upendo utatiririka ndani ya moyo kama kijito cha maji ya uzima, kinachotiririsha uzima wa milele. Upendo huu unapokuwa ndani ya moyo, mtendakazi hataona uchovu katika kazi ya Kristo” (Ellen White, Review and Herald, vol. 3, uk. 121, Feb. 13, 1894).
Shemasi mmoja, aliyefahamika kama mtu mwenye msaada na mvuto, alikuwa na tatizo kubwa la tabia ambalo mkewe na watoto pekee ndiyo walifahamu. Kazini au katika maburudisho yake na wengine, alikuwa mtu wa kirafiki sana unayeweza kutamani kukutana naye. Nyumbani, mara nyingi alikuwa mtu asiyevumilika. Anaweza kuwa na badiliko la tabia na mwenye kukasirisha. Nyakati nyingine hasira ilitawala, na alikuwa akiwatesa kihisia na kuwaadhibu sana watoto wake.
Shemasi huyo alifahamu hitaji lake. Alijichukia kwa kulipuka nyumbani. Alitambua kwamba alionyesha kitu kimoja mbele za watu na kuishi maisha tofauti nyumbani. Nyakati nyingine alitambua kwamba alipaswa kuhudhuria madarasa ya kutawala hasira, lakini aliogopa matokeo ya kukubali tatizo lake kanisani. Pia alifahamu kwamba alipaswa kupata ushauri, lakini alikatishwa tamaa na wazo la kumlipa mtu ili amsikilize. Kiburi chake kilimtenga na msaada aliohitaji. Alikuwa mtu wa dini bali si mtu wa kiroho – alihitaji kubadilishwa na kuwa na uwepo wa kudumu wa Roho Mtakatifu katika maisha yake.
Majira fulani ya mwaka, alikuja mhubiri katika mji wao na kuendesha mfululizo wa mikutano ya uamsho. Kwa sababu ya cheo chake kanisani, shemasi yule alihudhuria kila mkutano, japokuwa moyo wake ulikuwa kama jiwe. Maombi mengi yalitendeka katika mikutano hii, na Roho Mtakatifu alikuwa akitenda kwa njia za kimiujiza. Binti mmoja alifanya upya uhusiano wake na Yesu na kufanya ungamo la hadhara la dhambi zake, akiomba maombi na msaada wa kusanyiko lile. Mwanamke asiyekuwa Mkristo aliyehudhuria pamoja na rafiki aliyatoa maisha yake kwa Yesu. Maisha yalibadilika kadri watu walivyosogea mbele wakati wa wito kila usiku.
Usiku mmoja, karibia na miisho ya mikutano hiyo, wito ulipotolewa shemasi yule aliinuka na kwenda mimbarani. Akiwa na machozi usoni mwake, alielekea mbele pamoja na wengine walioitikia wito wa Mungu mioyoni mwao. Pale mbele ya kanisa, alianguka magotini, akainua mikono yake, na kusema kwa sauti, “Mungu, nisamehe mimi, mdhambi!” watu waliomfahamu shemasi yule walishangazwa kumsikia akiomba ombi lile mbele za watu, lakini hiyo haikuwa mwisho. Shemasi yule aliinuka, akageukia mkutano, na kusema, “Nina tatizo baya sana la hasira.
Mimi si mume na baba ninayepaswa kuwa. Ninahitaji kuungama dhambi zangu, kutafuta msaada, na nyumbani kwangu kuwa mwanaume ambaye wote mnamfahamu hadharani.” Muda huu mke na watoto wake walikuwa wamemzunguka huku wakilia na kumkaribia mume na baba yao. Washiriki wa kanisa nao walimzunguka, mchungaji aliweka mikono yake juu ya baba yule, na walikuwa na kipindi cha maombi cha ajabu usiku ule!
Shemasi yule alikuwa muaminifu kwa neno lake. Kwa msaada wa Mchungaji alipata mshauri, na pia alianza kuhudhuria madarasa ya kutawala hasira. Muhimu aidi, alianza masomo ya Biblia ya kila juma pamoja na mchungaji – si kuelewa mafundisho bali kutafuta uhusiano halisi na Yesu. Roho Mtakatifu alimbariki shemasi yule na alianza kumjaza kwa tunda la Roho. Si mke na watoto wake tu walioona badiliko bali washirki wa kanisa na jamii iliweza kuona pia. Shemasi alikuwa na Amani. Alikuwa mtu mwema Zaidi. Wema na upendo wake, hasa kwa mke na watoto wake, ulikuwa wazi kwa kila mtu. Furaha na mibaraka ya Yesu, kupitia kwa Roho Mtakatifu aliyedumu ndani yake, ilibadilisha nyumba ya shemasi yule kuwa mfano mdogo wa mbingu duniani.
Mafungu ya Biblia ya kuombea
Nyimbo Zinazopendekezwa:

- Wagalatia 5:19-23 – Kazi za mwili huondolewa kwa tunda la Roho Mtakatifu: upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, upole, kiasi.
- Yohana 13:35 – Watu watatufahamu kuwa ni Wakristo wa kweli kupitia upendo tunaouonyesha.
- 1 Petro 1:8 – Tutakuwa na furaha isiyoelezeka.
- Wafilipi 4:7 – Amani ya Mungu italinda mioyo na akili zetu.
- 2 Wakorintho 3:18 – Kwa nguvu ya Roho Mtatifu tunabadilishwa na kuwa na sura ya Yesu.
- Yohana 7:38 – Mito ya maji ya uzima itatiririka kutoka mioyoni mwetu.
- Mpendwa Yesu, ninataka kuakisi tabia yako kwa kila mtu ninayemfahamu na kwa wote ninaokutana nao. Nijaze kwa Roho wako Mtakatifu, na ruhusu tunda la roho ling’ae kutoka moyoni mwangu.
- Tafadhali nisaidie kuwa Mkristo halisi Zaidi nyumbani kuliko sehemu nyingine. Naomba wale wanaonifahamu vema waweze kukuona wewe Zaidi ndani yangu.
- Nifanye niwe mto wa mibaraka kadri ninavyoshiriki upendo, furaha, na Amani yako pamoja na dunia ninapoishi.
- Kadri ninavyotumia muda katika maombi na kujifunza Biblia, tafadhali nibatize Zaidi na Zaidi kwa Roho wako Mtakatifu. Naomba neema isiyo na kikomo itiririke kupitia kwangu na kuuendea ulimwengu unaoumia.
- Msifu Mungu, Ee moyo wangu, na liabudu jina lake takatifu. Furaha yake na ijaze nafsi yangu!
- Bwana, tafadhali safisha mioyo ya wale walio katika huduma wenye wasiwasi. Wakumbushe kwamba wanatenda mapenzi yako. Tafadhali waruhusu waone matunda ya kazi yao, hata ikiwa ni nafsi moja tu.
- Bwana, tunakumbuka waalimu wetu wa Shule ya Sabato. Tafadhali wasaidie kufahamu kazi yao ilivyo ya muhimu kwa watoto wetu.
- Bwana, tunaomba uongozi wako katika Vituo vingi vya Vivutio, programu za afya na familia, na klabu za Watafuta Njia duniani.
- Bwana, tafadhali tuonyeshe namna ya kutuma machapisho yaliyojazwa kweli (yaliyochapishwa na kielektroniki) katika jamii zetu. Tunaomba kwamba watu wayasome na Roho Mtakatifu awaonyeshe kweli ya Biblia.
- Tafadhali inua wainjilisti wa vitabu, wanafunzi wa kujitolea, waandishi, waliobobea katika masuala ya vyombo vya habari, na wategemezaji wa kifedha ili kusambaza maneno ya tumaini na uzima.
- Pia tunaomba wka ajili ya orodha yetu ya watu saba au Zaidi [taja majina kama inawezekana]
- Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:
Nyimbo Zinazopendekezwa:
- Kumtegemea Mwokozi #129,
- Yesu Nakupenda #29
- Mishale ya Nuru #164
No comments
Post a Comment