Siku 10 za maombi: Siku ya Sita - Jumatatu - (13/01/2020)

Zawadi za Roho Mtakatifu
Fungu Elekezi: “Basi pana tofauti za karama; bali Roho ni yeye yule. Tena pana tofauti za huduma, na Bwana ni yeye yule. Kisha pana tofauti za kutenda kazi, bali Mungu ni yeye yule azitendaye kazi zote katika wote. Lakini kila mmoja hupewa ufunuo wa Roho kwa kufaidiana.” 1 Wakorintho 12:4-7.

Ushuhuda 
“Ni usaidizi wa Roho Mtakatifu wa Mungu ndio unaoandaa watendakazi, wanaume na wanawake, kuwa wachungaji kwa watu wa Mungu… wale walio na Imani katika mtumishi wa kimbingu [Roho Mtakatifu] wataendelea. Watazawadiwa nguvu ya kuvita ujumbe wa kweli kwa uzuri mtakatifu” (Ellen White, Gospel Workers, aya. 96, 97).

Simu iliita ofisini kwangu mjini Albany, Oregon. “Je, huyu ni mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato?” sauti ya kike iliuliza. “Ndiyo.” Nilijibu. “Unapaswa kuja hospitali sasa hivi. Tuna mgonjwa hapa mwenye matatizo ya mapigo ya moyo. Tunadhani anaweza kufa, lakini hataki kuturuhusu kufanya cho chote hadi mchungaji kutoka kwenye Kanisa la Waadventista amuombee. Anaendelea kusisitiza kwamba mchungaji kutoka Kanisa la Waadventista akimuombea, atapona. Tafadhali njoo haraka!”

Nikiwa naendesha gari kuelekea hospitali, niliomba, “Bwana, nina wasiwasi kidogo kuhusu ugeni huu. Binti huyu anaendelea kuwaeleza watu kwamba mchungaji wa Kanisa la Waadventista akimuombea, atapona. Sote, wewe na mimi tunafahamu kwamba si kila muda unachagua kumponya mtu. Wauguzi na madaktari wale watasema nini ikiwa hutamponya Binti huyu?” Ilionekana kama bwana alijibu kwa kusema, “Unahofia nini?” “Ninahofia sifa yako njema,” nilisema. “Sasa, ngoja niweke hili sawa, “Bwana alionekana kunena. “Unahofia sifa yangu njema?” “SAWA,” niliendea, “Ninatambua hilo linaonekana jambo la kipuuzi kidogo, lakini watu watasema nini – binti yule atasema nini – ikiwa hutamponya?” Bwana alinena moyoni mwangu, “Ni wajibu wako kuwa mtii. Ni wajibu wangu kushughulikia sifa yangu njema.” “Upo sahihi,” nilisema. “Nitakuamini na kukuacha utende unachoona ni bora.”

Pale hospitalini nilikutana na wauguzi wanne nje ya chumba cha mgonjwa yule. “Je, wewe ndiye mchungaji wa Kiadventista?” muuguzi mmoja aliuza. “Harakisha uingie na kuomba ili tuweze kufanya kitu!” nilikwisha kufahamu kutokana na jina la binti huyu nililopewa na muuguzi kwamba si muumini wa kanisa langu au kanisa la karibu. Nilijiuliza kwa nini alisisitiza kuombewa na mchungaji wa Kiadventista, lakini huu haukuwa muda wa kuanzisha mazungumzo.
Mashine ya kuendeshe moyo wake ilionyesha mapigo ya moyo yanayobadilika badilika. Nilifahamu kwamba alikuwa katika matatizo. Nitembea kuelekea kando ya kitanda chake na kuushika mkono wake wa kuume. Aligeuka kidogo, akafumbua macho, na kuuliza, “Je, wewe ndiye mchungaji wa Kiadventista?” “Ndiyo,” nilisema. “Ukiniombea, ninafahamu kuwa nitaponywa,” alisema.

Huu haukuwa muda wa hubiri au kujifunza Biblia juu ya maombi kwa ajili ya wagonjwa. Kwa urahisi nilimuuliza, “Dada, upo tayari kumruhusu Yesu aamue kitakachotendeka leo hapa?” “Oh, ndiyo, mchungaji,” alisema, “lakini ninafahamu kwamba ukiniombea, nitaponywa!” Hivyo nilifumba macho yangu na kumuomba Mungu wa mbinguni kuonyesha nguvu zake na neema zake kwa binti huyu. Nilimuomba alitukuze jina lake mbele ya wauguzi na madaktari katika hospitali ile, na kwamba uponyaji wa binti huyu uwe ushuhuda kwa watu wengi. Nilimuomba Mungu amponye kama ndiyo yalikuwa mapenzi yake, kama kumponya kutaleta utukufu kwa jina lake, na kama ilikuwa kwa nia njema kwake. Nilimaliza ombi langu kwa jina la Yesu na kusema “Amina.” Nilipofumbua macho yangu, nilitazama mashine, na ilionyesha mtiririko thabiti wa mapigo ya moyo! Binti yule alishika mkono wangu kwa furaha na kusema, “Ninajisikia vizuri. Nimeponywa! Nilijua kwamba kama mchungaji wa Kiadventista akiniombewa, ningeponywa!”

Nilikumbuka namna Yesu alishughulika na hali kama hizi katika maisha yake, hivyo nilisema, “Dada, Imani yak imekuponya!” Nilimshukuru Mungu na kutoka katika chumba kile. Muuguzi alisema, “Tunaweza kuingia sasa?” Nilijibu, “Ndiyo, lakini sidhani kama anawahitaji tena.” Macho yao yalifumbuka Zaidi kwa mshangao, na wakakimbia kuingia kwenye chumba kile. Siwezi kukueleza kilichotokea tena baada ya pale kwani niliondoka. Sikutaka wauguzi au binti yule kunitazama kama mimi ndiye niliyemponya. Ilikuwa ni karama ya uponyaji iliyotolewa na Roho Mtakatifu kwa ajili ya binti yule kwa wakati ule.

Mafungu ya Biblia ya Kuombea:

  1. 1 Wakorintho 12:9 – Karama ya uponyaji imetajwa. Bwana ana njia nyingi za kuponya watu, na anataka kudhihirisha nguvu yake ya uponyaji kupitia watu wake.
  2. Waefeso 4:11-13 – Roho Mtakatifu anataka kutoa karama nyingi kwa watu wake. Mungu ana mpango kwa ajili yako pia.
  3. Luka 5:17 – Nguvu ya Bwana ipo ili iponye. 
  4. 1 Wakorintho 14:1, 13 – Tamani karama za roho na omba kwamba uzipokee.
  5. Ufunuo 1:10 – Roho Mtakatifu anapokuja juu yetu, tunaweza kumsikia Mungu kwa njia mpya na yenye nguvu.
Mapendekezo ya Maombi
  1. Nipo hapa, Bwana, nitumie katika huduma kila. Nijaze kwa Roho yako na kunijaza karama zako.
  2. Mpendwa Yesu, ninataka kufanya badiliko kwa ajili yako katika dunia hii. Sifurahishwi na kukaa tu kanisani. Nipatie nguvu ya Roho wako kupitia karama unazonichagulia ili niweze kushinda nguvu za dhambi katika dunia hii.
  3. Bwana, ongeza karama zetu kwa elimu, semina, uzoefu, na maombi. Tunaweka wakfu talanta zetu kwako na kwa unyenyekevu tunaomba kwamba uongeze mibaraka yako isiyo ya kibinadamu ili kwamba injili isonge mbele kwa nguvu.
  4. Tunaomba kwa ajili ya shule 8,208 za Kiadventista zenye wanafunzi karibia milioni 2. Hebu shule hizi zifundishe daima kweli za Biblia na kuwaongoza vijana katika utume na huduma.
  5. Bwana, tupatie hekima ya kufikia tamaduni zisizo na dini ambazo hazina shauku katika dini. Mruhusu Roho wako Mtakatifu avunje kuta zinazoizunguka mioyo isiyokuwa na dini.
  6. Tunaomba kwa ajili ya makundi ya watu katika Asia ambayo hayana historia ya Ukristo. Tupatie hekima ya kuyafikia mahitaji yao.
  7. Bwana, tafadhali tia msukumo kwa Waadventista wa Sabato ulimwenguni wa kuomba kuliko ilivyowahi kutokea hapo kabla. Tusiadie kutsihi pamoja kwa ajili ya mvua ya masika ya Roho Mtakatifu. Tunaomba ukamilisho ulioahidiwa wa Yoeli 2, Hosea 6, na Matendo 2.
  8. Tunaomba kwa ajili ya makundi 541 ya watu katika nchi 18 za Divisheni ya Kusini mwa Afrika-Bahari ya Hindi. Tadhali wangoze katika kweli ya Kibiblia.
  9. Pia tunaomba wka ajili ya orodha yetu ya watu saba au Zaidi [taja majina kama inawezekana]
  10. Mahitaji ya kuombea ya kanisa mahalia:

Nyimbo Zinazopendekezwa

  1. Tupe Moto wa Uhai #81,
  2. Nijaze Sasa #40
  3. Ninaye Rafiki #49

No comments

Powered by Blogger.